ASKOFU SANGU ATANGAZA RASMI PAROKIA MPYA YA LAGANGABILILI NA KUMSIMIKA PADRE PETER KIJA KUWA PAROKO WA KWANZA WA PAROKIA HIYO.

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, leo Ijumaa tarehe 05.07.2024, ametangaza na kufungua rasmi Parokia mpya ya Lagangabilili, huko wilayani Itilima mkoani Simyu.
Kufuatia kuanzishwa kwa Parokia mpya ya Lagangabilili, Askofu Sangu amemtangaza na kumsimika Padre Peter Kija kuwa Paroko wa kwanza wa Parokia hiyo mpya, ambayo iko makao makuu ya Wilaya ya Itilima.
Parokia hiyo inalifanya Jimbo la Shinyanga kuwa na Jumla ya Parokia 40, ambapo kati ya hizo, 14 zimeanzishwa na Askofu Sangu kwa kipindi chake cha miaka 9 tangu alipoanza kulichunga Jimbo la Shinyanga mnamo mwaka 2015.
Misa ya kufunguliwa kwa Parokia mpya ya Lagangabilili ambayo imetokana na kumegwa kwa sehemu ya Parokia kongwe ya Kilulu na maeneo machache ya Parokia ya Ng'wandoya, imehudhuriwa na Mapadre, Watawa na waamini kutoka sehemu mbalimbali za Jimbo, pamoja na viongozi wa Serikali wakiwemo Mbunge wa Itilima Njalu Silanga na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Anna Joram Kidarya

 

Previous Post Next Post