Askofu wa JimboKatoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho Jumapili tarehe 14.07.2024, atafanya ziara ya siku moja katika Parokia ya Kilulu Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Askofu Padre Paul Mahona, Askofu Sangu ataongoza Misa ya Kipaimara na kuwaimarishwa waamini zaidi ya 100, ambayo itaanza saa 4:00 asubuhi.
Askofu Sangu atawasili Parokiani Kilulu kesho asubuhi, ambapo pia atapokea michango ya kulitegemeza Jimbo kutoka kwa waamini.