Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho Alhamisi tarehe 11.07.2024, atafanya ziara ya chungaji ya siku moja katika Parokia ya Sayusayu Wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Kwa mujibu wa Katibu wa Askofu Padre Paul Mahona, ziara hiyo itakwenda pamoja na utolewaji wa Sakramenti ya Kipaimara kwa waimarishwa zaidi ya 200, kupitia adhimisho la Misa takatifu ambayo itaanza 4:00 asubuhi.