BENARD BENSON WEREMA ATOA AHADI BAADA YA KUSHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA SHINYANGA

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benardd Benson Werema akizungumza baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti katika nafasi hiyo leo Alhamisi Julai 4,2024

Na Mapuli Kitina Misalaba

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya  ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga, wamemchagua Benardd Benson Werema kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Shinyanga, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Clement Madinda ambaye alipata uteuzi kwenye utumishi wa Umma.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo leo Julai 4,2024 msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe.  Juma Chikoka amemtangaza Benard Benson Werema kuwa mshindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura 252 dhidi ya wagombea wenzake watatu

Msimamizi huyo wa Uchaguzi amesema jumla ya wagombea walikuwa wanne  ambapo amewataja wengine watatu kuwa  ni Makamba Mussa Lameck ambaye amepata kura 78,akifuatiwa na Irene Masakilija aliyepata kura 19,huku Severine Leonald Mbulu amepata kura 12,na kwamba  kura zilizopigwa ni 367,  kura zilizoharibika ni 6 na kura halali zilikuwa 361.

Akizungumza  baada ya kupata ushindi huo Bwana Benard Benson Werema pamoja na mambo mengine amewashukuru wajumbe wa Mkutano huo na kuahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi,uadilifu,kwa kushirikiana na viongozi na wanachama wa UVCCM, Chama na  jumuiya  zake zote.

“Ninawashukuru sana vijana wenzangu mmenipa imani ambayo inaenda mpaka 2027 Mungu akitujalia uhai nifikishieni salamu kwenye Halmashauri zetu huko, ninawaahidi sitawasariti vijana wala sitawauza kwa vipande vya 20 kutoka kwa mtu yoyote nawahakikishia kuwa sisi vijana tutawaheshimu watu wote, tutazingatia kanuni, tutasikiliza miongozo na tutatekeleza maagizo tutakayopewa na viongozi wetu”.

“Vijana nendeni mkaendelee kukisemea Chama cha Mapinduzi nendeni mkamsemee mheshimiwa Rais, wamemeeni waheshimiwa wabunge kwa mambo wanayotufanyia na waheshimiwa madiwani ili wananchi waweze kutambua maendeleo yaliyopo”.amesema Werema

Aidha  Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo, amepongeza uchaguzi huo kwa kufanyika kwa Amani na Utulivu,huku akiwaasa  Vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye  uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji utakaofanyika baadaye  Mwaka huu 2024.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe.  Juma Chikoka akizungumza.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe.  Juma Chikoka akizungumza.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benardd Benson Werema akizungumza baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti katika nafasi hiyo.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Benardd Benson Werema. 

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo akizungumza leo Alhamis Julai 4,2024. 

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bi. Odilia Batimayo akizungumza leo Alhamis Julai 4,2024. 

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya  ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya  ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Shinyanga.





Previous Post Next Post