Na Mapuli Kitina Misalaba
Chama cha Girl Guide kimezindua
rasmi kampeni maalum Mkoani Shinyanga
inayolenga kuwawezesaha wasichana na wanawake kujiamini na kujithamini
katika maisha yao ya kila siku.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika
katika shule ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi
ya wawakilishi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda, Tanzania, Bangladesh,
Zimbabwe pamoja na Madagascar.
Msimamizi wa miradi ya Girl Guide
kutoka makao makuu, Valentina Gonza amesema chama hicho kipo nchi zaidi ya 52
Duniani ambapo pia amesema mpaka sasa zaidi ya wanachama milioni kumi wasichana
na wanawake wamejiunga na chama hicho.
Gonze amesema Girl Guide ni chama
cha kujitolea ambacho hakifungamani na dini wala vyama vya siasa huku akitaja
malengo ya chama hicho ikiwemo kuwawezesha wasichana na wanawake kufikia ndoto
zao.
“Girls Guide ni chama
cha kujitolea ambacho hakifungamani na dini yoyote kwahiyo unaweza ukawa mkristo,
unaweza ukawa mwislamu na unaweza ukawa
mpagani lakini pia chama hichi hakifungamani
na vyama vyovyote vya siasa kwahiyo mtu yoyote anaweza akawa mwanachama kutoka
sehemu yoyote, lakini pia ni chama ambacho hakichagui kazi au taaluma unaweza
ukawa mwalimu, unaweza ukawa mwanafunzi, unaweza ukawa daktari, unaweza ukawa
nesi, unaweza ukawa mjasiliamali unaweza ukawa mkulima kwahiyo ni chama ambacho
mtu yoyote anaweza kujiunga”.
“Chama hiki kimejikita zaidi kuwajengea uwezo watoto wa kike
na wanawake waweze kujitegemea, kujiamini, kuwa wazalendo na kuwawezesha waweze
kufikia ndoto zao kwenye maisha yao kwa kupitia mafunzo ambayo yanatolewa na
Girls Guide na mafunzo haya yapo kuanzia umri mdogo wanachama wetu ni kuanzia
umri wa Miaka sita (6) na haya mafunzo yamegawanyika kulingana na umri husika
kwahiyo watoto wenye umri kuanzia Miaka sita (6) hadi tisa (9) wanamafunzo yao maalum
ambayo yanaendana na mahitaji ya huo umri”.
“Pia kuanzia umri wa Miaka kumi (10) hadi kumi na mbili (12)
wanamafunzo yao maalum kwahiyo kila kundi lika linamafunzo maalum ambavyo
yameshaandaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wasichana”.
“Girls Guide ni chama ambacho kipo nchi zaidi ya 52 Duniani
na kuna wanachama zaidi ya Milioni kumi wanawake na wasichama katika nchi
mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania, Bangladesh, Zimbabwe,
Madagascar na nchi zingine za afrika na Duniani kwahiyo tunapokuwa na huu umoja
wetu inatufanya tuweze kujifunza vitu mbalimbali kujifunza tamaduni za wenzetu kujifunza
jinsia gani wenzetu wanapambana na changamoto ambazo wasichana na wanawake
zinawakabili kama vile masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na elimu ya
utunzaji wa mazingira kwahiyo kwenye Girls Guide tunawajengea watoto wa kike uwezo
wa kuwa na mifumo ambayo itatufanya sisi kuwa salama zaidi”.amesema Gonze
Ametumia nafasi hiyo kuwaomba
wasichana na wanawake kujitokeza ili kujiunga na Girl Guide na kwamba waweze kunufaika na
fursa zinazojitokeza kupitia chama hicho.
Kampeni hiyo pia imelenga kutoa
elimu katika jamii, kuachana na dhana potofu ambazo zimekuwa zikihusishwa kwa
watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali ili jamii kutambua na kuthamini mchango
wa watu wenye ulemavu na kwamba waweze kutoa fursa zawa na watu wengine.
Kwa upande wake mkufunzi wa chama
cha Girl Guide Mkoa wa Shinyanga Veronica Marwa amesema matarajio ya kampeni
hiyo kwa Mkoa wa Shinyanga ni kuwafikia wasichana elfu tatu (3000) kuanzia Julai
2 hadi Julai 6 Mwaka huu 2024 katika shule za msingi, sekondari na vyuo na
kwamba zoezi hilo ni endelevu.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
msingi Buhangija wameshukuru kwa elimu hiyo huku wakiahidi kushiriki kikamilifu
katika kampeni za Girl Guige ili kufikia malengo yao.
Chama cha Girl Guide ni chama kinachompa kila mtu uhuru na nafasi ya
kuzungumza na kwamba kinaendesha mafunzo mbalimbali yakiwemo mafunzo ya hedhi
salama, mafunzo ya kuwawezesha wasichama na wanawake kujiamini na kujithamini,
kuheshimiana na kuepukana na mila potofu zilizopo kwenye jamii.
Msimamizi wa miradi ya Girl Guide
kutoka makao makuu, Valentina Gonza akizungumza.
Mkufunzi wa chama cha Girl Guide Mkoa
wa Shinyanga Veronica Marwa akizungumza.