Na Mwandishi Wetu
Sakata la Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha,Justin Nyari na aliyeshinda tuzo katika Mahakama ya Rufaa dhidi ya Kampuni ya The Guardian limeingia katika sura mpya baada Wakili wa Mfanyabiashara huyo kusema kuwa Dalali wa Kampuni ya First World Investment ya Jijini Arusha ndio kikwazo cha utekelezaji wa uuzwaji wa mali za kampuni hiyo ya vyombo vya habari.
Mahakama ya Rufaa iliiamuru Kampuni The Guardian ya Jijini Dar es Salaam kumlipa Justin Nyari Mfanyabiashara wa Madini ya Tanzanite kiasi cha shilingi milioni 410 ndani ya siku 14 ilizopewa na Mahakama hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kituo Jumuishi Mkoani Arusha,Wakili wa Nyari,Kelvin Kagilwa alisema kuwa Dalali,Allan Mollel wa Kampuni ya First World Investment aliyeteuliwa na Mahakama ameshindwa kuelewa ni kwa nini Dalali huyo hakuonekani Mhakamani hapo na hakuna sababu zilizotolewa mbele ya mahakama.
Wakili Kagilwa alisema mara ya mwisho Mahakamani hapo Dalali Mollel aliomba wiki mbili za kufuatilia nyaraka za Mtathimini Mkuu wa Serikali kwani alipeleka nyaraka zote kwake ikiwa ni pamoja na nakala ya barua ya mahakama Kuu.
‘’Leo tulipaswa kupataa jibu kama thamini ya mali ya The Guardin imefanyiwa tathimini au la lakini Dalali hayuko na hakuna taarifa za kutoonekana Mahakamani hapo na tumeshindwa kulikoni yeye kushindwa kufika Mahakamani’’alisema Wakili Kagilwa
Dalali Mollel alipotafutwa kujibu ni kwa nini hakuwepo Mahakamani,Mollel alisema kuwa alipata dharura ya msiba na alitoa taarifa kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na pia yeye sio kikwazo kufanya utekelezaji wa amri ya Mahakama kwa mshinda tuzo.
Mollel alisema yeye anasubiri majibu kutoka kwa Mthamni Mkuu wa Serikali kwani mara ya mwisho aliambiwa kuwa kiongozi huyo alikuwa katika maonyesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaama kwa hiyo hakukuwa na chochote kilichoendelea.
Hata hivyo Mthamini Mkuu wa Serikali,Evalina Mfula alisema kuwa sio kweli kwamba yeye alikuwa kwenye maonyesho ya Saba Saba lakini ofisi iko waziwazi masaa yote ya kazi hata kama yeye yuko njee ya ofisi hivyo dalali anapaswa kukueleza ukweli.
Mfula aliendelea kusema kuwa hana nyaraka zozote kutoka Mahakama Kuu Arusha juu ya suala la nyari na The Guardin hivyo alihitaji kupata tathimini ya awali juu ya mali za The Guardin.
‘’Dalali aseme ukweli aache uongo ni vema nikapata nyaraka zote ili nijue jambo hili limekwamia wapi na sio kutoa visingizio katika ofisi yangu wakati sio kweli’’alisema Mfula
Kampuni ya First World Investment may 16 mwaka huu alimwandikia Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha kuwa amefanya kazi ya awali ya utekelezaji wa oda ya Mahakama Kuu aliyoitoa may 6 mwaka huu ya kuupa taarifa uongozi wa Kampuni ya The Guardian juu ya kutakiwa kumlipa Nyari kiasi hicho cha fedha ndani ya siku hizo.
‘’Tafadhali rejea amri{Order} ulioitoa may 6 mwaka huu,Utekelezaji wake nikaufanya may 13 mwaka huu kwa kufika kwenye eneo husika ‘’Bulding on Plot no 122 Mikocheni service Trade Area Dar es Salaam in c.t.no 47632 in the name of Guardian limited ‘’
‘’Taratibu za uthamini zinaendelea nitawasilisha taarifa zitakapokuwa tayari na siku 14 za taarifa zitaisha may 27 mwa huu’’ naomba kuwasilisha taarifa ya awali ya utekelezaji kwa hatua zako muhimu’’ ilisema sehemu ya barua ya Mollel
Mwaka 2000 kampuni ya The Gurdian kupitia vyombo vyake vya habari viliandika mfanyabiashara Nyari alikuwa akipinga wawekezaji kwenye madini ya Tanzanite kwa kuhamashisha vijana maarufu kwa jina la wana Apolo hatua ambayo ilimfanya Mfanyabiashara huyo kupata usumbufu wa kibiashara kwa wateja wake wa ndani ya nchi na nje na kuamua kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga hilo na The Guardian Kuthibitisha hilo Mahakamani vinginevyo imsafishe ama kumlipa fidia ya shilingi bilioni moja kwa kumchafua.
Nyari ambaye wakati huo alikuwa akitetewa na Wakili Mkongwe Jijini Arusha,marehemu Loamu Ojare alishinda kesi hiyo Mahakama Kuu na Kampuni ya The Guardian iliamuriwa kumlipa Nyari shilingi milioni 700 badala ya shilingi bilioni moja lakini Kampuni ya uwakali ya Ngallo Advocate iliyokuwa ikiitetea The Guardian ilikata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu hiyo lakini ilishindwa mbele ya Majaji watatu na Mahakama hiyo kuamuru Nyari kulipwa shilingi milioni 410 kwa kuchafuliwa.