Diwan wa Kata ya Buhongwa Mhe,Benard Joseph Kabadi amewataka Watumishi wanaotaka Maji na kumuuzia Mtu Mmoja Mmoja kuacha mara Moja maana Shida ya Maji Kwa Wananchi wa Buhongwa ni kubwa
Akizungumza Leo katika Mkutano wa kawaida uliowakutanisha wazazi na waalimu wa Shule ya Msingi Buhongwa amesema Wananchi waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi Chini ya Dkt Samia Suluhu Hassani Ambae ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Lakini pia Mhe, Benard Joseph Kabadi amepongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe,Amina Nassor Makilagi Kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha Anawatafuta wadau Ili kuunga Mkono jitihada za Serikali
Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Buhongwa Oliver Benedicto rweyemela ametoa Pongezi Kwa Diwani wa Kata iyoo Kwa Kuitisha Mkutano huo wa Kawaida Ili kuongeza jitiada za Serikali" Sisi shule yetu Imepata Fedha Nyingi Kwa ajiri kuboresha Shule kujenga na kujenga Uzio ambacho kilikuwa ni kilio Cha Mda Mrefu