DKT SAMIA AWAKOMBOA WAKULIMA WA MAHINDI MKOANI KATAVI ,MALALAMIKO KUHUSU BEI ELEKEZI YA MAHINDI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Samia Suluhu Hassan imetatua changamoto ya bei elekezi ya mahindi mkoani Katavi iliyolalamikiwa kwa muda.

Kupitia Wizara ya Kilimo na Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Hussein Mohamed Bashe amesema bei ya wakulima kuanzia leo Vituo vyote vya ofisi ya wataalamu wakala wa Taifa uhifadhi wa chakula  (NFRA),Vijijini mahindi sio 500 ni 600 kwa kilo na makao makuu ya miji ni 650.

Previous Post Next Post