JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LIMEFANIKIWA KUMKAMATA MSICHANA MMOJA (MADUKI SABUNI) MWENYE UMRI WA MIAKA 16, KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kumkamata  Msichana mmoja aliyejitambulisa kwa jina la Maduki Sabuni  mwenye umri wa Miaka 16,kwa tuhuma za kuiba Mtoto

 Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga,kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Janeth Magomi amesema  Mtoto huyo aliibiwa tangu Julai 18, 2024 katika kituo cha Mabasi Mjini Kahama,wakati Mama yake Bi Magdalena Silas akiendelea na shughuli za utafutaji

 Amesema Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa za wizi wa mtoto huyo, lilianza kufanya upelelezi na kwamba Julai 21 mwaka huu, huko maeneo ya ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita, lilifanikiwa kumkamata binti huyo Maduki Sabuni  akiwa na mtoto huyo mwenye umri wa miezi tisa

 Amesema mtoto huyo amepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya uchunguzi wa afya  yake na baadaye atakabidhiwa kwa mama yake mzazi.

 Kamanda  Magomi ameonya wale wote wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa watoto, kwani amesema tukio hilo linakuwa la pili kutokea katika kipindi cha miezi miwili.

TAZAMA VIDEO

Previous Post Next Post