Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuimarisha ulinzi na
usalama kwa kushirikiana na Jamii katika kubaini, kuzuia na kutanzua
uhalifu kwa kufanya doria, misako, operesheni na kutoa elimu kwa
Wananchi kuanzia Juni 26, 2024 mpaka Julai 24, 2024.
Kwa kipindi tajwa hapo juu Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
limefanikiwa kukamata Watuhumiwa watatu wakiwa na vifaa vya
kutendea uhalifu ambavyo ni Gari 01 aina ya TOYOTA CROWN
ndogo nyeupe, vipande 20 vya Dhahabu, brashi 26 za kusugulia
Dhahabu pamoja na mizani 03.
Lakini pia katika misako mingine limefanikiwa kukamata pombe ya
moshi lita 176, Pikipiki 14, bhangi kilogramu 65, Mafuta ya dizeli lita
20, Bati 10, Shock-up za pikipiki 04, Bomba 03 za chuma, Spana 22,
radio 03, POS mashine 01, Simu 05, Laptop 01, kinu kimoja cha
mashine ya kusaga, TV 01, Sola panel 01, Betri ya sola 01, mzani 01,
Invetor 01, Kaboni mfuko 01 na deki 01 upelelezi unaendelea na mara.
MAFANIKIO YA KESI MAHAKAMANI
Jumla ya kesi 15 zimepata mafanikio ambapo kesi 01 ya mauaji
mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo cha miaka 05 jela, kesi 05 za wizi
washtakiwa 05 walihukumiwa kifungo cha miezi sita mpaka miaka
minne jela, kesi 01 kupatikana na madawa ya kulevya aina ya bhangi
mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo cha miaka 03 jela, kesi 01
shambulio la aibu mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili
jela, kesi 01 kula njama ya kufanya mauaji washtakiwa wanne
walihukumiwa kifungo cha mwaka 01 jela, kesi 01 ya kufanya fujo
mshtakiwa 01 alihukumiwa kifungo cha miezi 08 jela na kesi 05
kuingia kwa jinai washtakiwa 06 walihukumiwa kifungo cha miezi
mitatu jela.
MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia kikosi cha Usalama
barabarani limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 3,943 kwa
mchanganuo ufuatao:- makosa ya magari ni 2,752 na makosa ya
bajaji na pikipiki ni 1,191 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za
papo kwa hapo. Pia madereva wawili wamefungiwa leseni zao kwa
kipindi cha miezi mitatu kwa kosa la kuendesha gari kwa mwendokasi
zaidi ya Kilomita 100 kwa saa.
Aidha kwa upande wa utoaji wa elimu Jeshi la Polisi limefanikiwa
kufanya jumla ya mikutano 71 ya uelimishaji kwa Wananchi, Wadau,
elimu mashuleni, nyumba za ibada na vyombo vya habari na hii
imesaidia kupunguza makosa ya ukatili na uhalifu mkubwa baada ya
wananchi kupata uelewa wa kutosha kuhusiana na makosa ya
kiuhalifu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashukuru Wananchi kwa
kuendelea kutoa ushirikiano madhubuti katika kuhakikisha Usalama
wa Mkoa wa Shinyanga unakuwa shwari sambamba na kupokea
elimu inayotolewa. Pia linatoa wito kwa madereva pamoja na
wananchi wote kuendelea kuti na kufuata Sheria na halitasita
kumchukulia hatua mtu yeyote atakayekiuka Sheria za nchi.