Na Mapuli Kitina Misalaba
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Wilaya ya Shinyanga mjini ikiongozwa na
Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Mhe. Anord Makombe imeridhishwa na miradi mitano (5) iliyotekelezwa na Mamlaka
ya majisafi na usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) katika Halmashauri ya Manispaa
ya Shinyanga.
Hayo yamebainishwa leo Jumatano
Julai 24,2024 baada ya kamati hiyo kutembelea na kukagua miradi hiyo mitano yenye thamani zaidi ya bilioni
moja.
Akizungumza Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Mhe. Anord Makombe ameipongeza SHUWASA kwa
kuimarisha huduma ikiwa ni pamoja na kutoa
taarifa kwa wakati na kushughulikia changamoto za wateja huku akiwahimiza
kuendeleza ushirikiano huo.
“Mimi niwapongeze SHUWASA mnajitahidi sana lakini lipo eneo
ambalo tumeona mmefanya vizuri japo halijafika kwa asilimia mia moja pamoja na ubora wa huduma za SHUWASA, mamlaka ya
majisafi SHUWASA tumeona mtandao karibia kila eneo umefika lakini kwenye
changamoto za kukatika kwa maji mnajitahidi kutoa taarifa mimi niwaombe tu
muendelee kuongeza wateja kwa sababu tunapoongeza wateja na kipato kinaongezeka
ili mamlaka iweze kustawi zaidi ya hapo tuendelee kuwa na ushirikiano tufanye
kazi wote kama timu”.amesema Makombe
Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias
Ramadhan Masumbuko naye ameipongeza SHUWASA kwa kuyafikia maeneo yote ya
Manispaa ya Shinyanga huku akiwasisitiza kuendelea kuzingatia suala la usafi
katika maeneo ya miradi pamoja na kushughulikia kwa haraka changamoto pale
zinapojitokeza kwa wananchi.
“Nawapongeza sana kwa sababu maeneo yote ya Manispaa
yamefikiwa na maji kwahiyo vimebaki tu vile viunganishi kutoka hapa kwenda pale
lakini kazi mnafanya vizuri na mnahitaji pongezi kubwa sana niendelee kuwatia
moyo watumishi wa SHUWASA kazi wanazozifanya ni kubwa maana zinaonekana”.amesema Mhe. Masumbuko
Wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya
Shinyanga mjini pamoja na mambo mengine wameridhishwa na miradi hiyo mitano
ambayo wameitembelea huku wakiisisitiza mamlaka hiyo kuendeleza ushirikiano
uliopo kwao na wateja wao.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga
wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kutatua changamoto ya maji ambayo ilikuwa ni kero kwao huku
wakiipongeza SHUWASA kwa kuendelea kuwashirikisha katika hatua mbalimbali kwa
lengo la kuimarisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya ameitaja
miradi ambayo imetembelewa na kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini,
miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa mtandao wa bomba na vituo vya kuchotea maji
kijiji cha Bugwandege ambapo amesema mradi huo tayari umekamilika na kwamba
wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.
Amesema mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba
kijiji cha Bugimbagu umekamilika kwa asilimia mia moja ambapo tayari wananchi
wanapata huduma ya majisafi na salama, ujenzi wa mtandao wa bomba na kituo cha
kuchotea maji kijiji cha Magwata mradi umekamilika pamoja na upanuzi wa mdandao
wa bomba Ngelegani, Ndala na Butengwa tayari wananchi wanapata huduma ya
majisafi na salama.
Pia amesema mradi wa ujenzi wa mdandao wa bomba
na kituo cha kuchotea maji kijiji cha Mwanubi umekamilika na wananchi wanapata
huduma ya majisafi na salama huku akiendelea kuwakumbusha wananchi kutunza
miundombinu ya miradi hiyo ili iweze kuduma.
Viongozi na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wakipata maelezo ya miradi kabla ya kuanza ukaguzi.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya akifungua
chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na vituo vya
maji kijiji cha Bugwandege Manispaa ya Shinyanga.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga
ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na
vituo vya maji kijiji cha Bugwandege Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa
usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akielezea chemba ya Valve ya mtandao wa maji.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya
ya Shinyanga mjini ikikagua Gati la maji Bugwandege leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya
ya Shinyanga mjini ikikagua Gati la maji Bugwandege leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa
usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akiandika ushauri unaotolewa na mstahiki
meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya na Kaimu
mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa wakiandika
ushauri unaotolewa na mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias
Ramadhan Masumbuko leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa
usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akielezea chemva ya Valve ya mtandao wa maji.
Kaimu mkurugenzi wa SHUWASA mhandisi Reuben Mwandumbya
akielezea mradi huo katika kijiji cha Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya
Shinyanga.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya
ya Shinyanga mjini ikiendelea kukagua Gati la maji Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ikiendelea kukagua Gati la maji Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga
ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba na
vituo vya maji kijiji cha Magwata Nhelegani Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Mhe.
Anord Makombe akiwasili katika Gati la maji
kijiji cha Magwata manispaa ya Shinyanga.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akipata ufafanuzi katika Gati la maji Magwata Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Shinyanga
ikikagua chemba ya Valve ya mtandao wa bomba la maji katika mradi wa bomba kijiji cha Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga leo Julai 24,2024.
Kaimu mkurugenzi usambazaji maji na usimamizi wa
usafi SHUWASA Mhandisi Uswege Musa akitoa maelezo ya mradi katika Gati la maji
Bugimbagu kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya
ya Shinyanga mjini ikiendelea na ukaguzi wa miradi.