Katibu siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Geita Ndg Gabriel Nyasilu ameitaka jamii ya wana kijiji cha Chankolongo kata ya Bukondo Wilayani Geita kukemea na kufichua waharifu wanaojihusisha na ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kwa kuwafichua kwenye vyombo vya Dola Kabla hawajatekeleza ukatili huo ambao umekuwa ukidhurumu haki za kuhishi kwa Watu wenye ulemavu huo.
Nyasilu Ameyasema hayo wakati wa Hafra ya kuzindua nyumba ya kuishi ya Mzee Mussa Kabaka ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Chankolongo kilichopo Kata ya Bukondo Wilayani Geita.
Amesema walemavu wa ngozi wana haki yakuishi ,Mungu kawaumba ili wafurahie maisha hivyo ni wajibu wa jamii nzima kuhakikisha wanawalinda watu hao.
"Mtu kuzaliwa Mlevu wa ngozi akupanga ni Mungu ndiye amepanga lakini kuna Watu Ambao wamekuwa Awana hofu ya Mungu wamekuwa wakiwadhuru wa madai watapata mali niwaombe tupinge vikali dhana hizi potofu"Alisema Gabriel Nyasilu.
Katika hatua nyingine Mwenezi Gabriel Nyasilu amewataka wanachi wa kijiji hicho kujitokeza kwa wingi wakati wa kujiandikisha kwenye Daftari la makazi ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopo mbele yetu Mwaka huu 2024.
Huku akiikumbusha jamii ya kata ya Bukondo na Geita kwa ujumla kuwa uchaguzi huu unaotokana na Mfumo wa vyama vingi usitumike kuwagawa na kuwagombanisha , Kwani
Wote ni watanzania kamwe wasikubali na kugawanywa na kugombana kwa sababu ya vyama vyao.
"Niwaombe Sana twende tukashiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa,Vijiji na Vitongoji kwa Amani ,upendo huku tukiilinda Amani ya nchi yetu"Alisema Gabriel Nyasilu .
Kwenye Ufunguzi huo Nyasilu ameongoza Harambee na kuwezesha upatikanaji wa Tsh 9,000,400/= Kwa ajiri yakusaport ujenzi wa Nyumba hiyo huku yeye Mwenyewe akichangia kiasi cha Tsh 500,000/=
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kijiji cha Chankolongo Mzee Mussa Kabaka amempongeza na Kumshuru katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita kwa kukubari wito wa kuwa Mgeni Rasmi katika hafra ya uzinduzi wa Nyumba yake.
Mwisho..