MAANDAMANO UGANDA LEO, WABUNGE WAKAMATWA


KAMPALA: Wabunge watatu wa upinzani nchini Uganda wamekamatwa na kuwekwa kizuizini kuelekea maandamano ya kupinga rushwa yaliyokuwa yamepigwa marufuku, yaliyopangwa kufanyika leo, Polisi wamesema,

Kiongozi wa upinzani nchini humo Bobi Wine amesema vikosi vya usalama vyenye silaha vimezingira makao makuu ya chama chake cha National Unity Platform (NUP) yaliyopo kitongoji cha Kavule, katika mji mkuu, Kampala.Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine.

Hatua hiyo inakuja siku mbili baada ya Rais Yoweri Museveni, ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa karibu miongo minne, kuonya kuwa watu waliopanga kushiriki maandamano hayo “wanacheza na moto.”


“Wabunge watatu na watu wengine saba wamefikishwa mahakamani, wakishtakiwa kwa makosa mbalimbali na kuwekwa kizuizini,” msemaji wa polisi wa Uganda Kituuma Rusoke ametangaza bila kutoa maelezo zaidi kuhusu mashtaka hayo.

Amewataja wabunge waliokamatwa kuwa ni Francis Zaake, Charles Tebandeke, na Hassan Kirumira — wote wakiwa ni wanachama wa upinzani wa NUP na kusema watafikishwa tena mahakamani Julai25 kwa ajili ya kusikiliza maombi yao ya dhamana.Wanajeshi na Polisi wa Uganda wakiwa wamezunguka makao makuu ya NUP jiji Kampala.

Kukamatwa kwa watu hao kumekuja baada ya waandamanaji kuapa kufanya maandamano ya kupinga rushwa, yaliyohamasishwa na maandamano ya kupinga serikali nchi jirani ya Kenya.

Lakini Msemaji wa polisi Rusoke amesema Polisi haitaruhusu maandamano yatakayohatarisha amani na usalama wa nchi.

Ametetea kuwepo kwa polisi na wanawajeshi kuzunguka makao makuu a chama cha Wine, NUP jijini Kampala akisema ni sababu za kiusalama.

Msemaji wa NUP Joel Ssenyonyi amesema wabunge hao watatu wamefunguliwa mashitaka ya makosa ya usalama barabarani na kuwazuiwa maafisa wa poilisi, mashitaka ambayo wamekanusha.


“Wamefikishwa mahakamani muda wa jioni ili wasipate dhamana na wote wamerejeshwa rumande,” amesema.


The anti-graft movement in Uganda has taken inspiration from anti-government demonstrations that have shaken neighbouring Kenya for more than a month, led largely by young Gen-Z Kenyans.


Harakati za kupinga rushwsa nchini Uganda zimepata hamasa kutoka kwa maandamano ya kupinga serikali ambayo yameitikisa nchi jirani ya Kenya kwa zaidi ya mwezi mmoja, yakiongozwa kwa kiasi kikubwa na raia vijana wa kizazi cha Gen-Z wa Kenya.
Previous Post Next Post