Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa CCM kata ya Lyamidati.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe.
Zawadi Lufungulo Mwasha akizungumza kwenye mkutano leo Julai 10,2024.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan pamoja na Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum kwa kufanikisha
utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba
itapunguza au kumaliza kabisa changamoto za wananchi.
Wametoa pongezi hizo leo Jumatano Julai 10, 2024
kwenye ziara yao ya kutembelea kata za Halmashauri hiyo kwa lengo la
kuhamasisha wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya zake kushiriki kikamilifu
katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu
2025.
Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga wameendelea na ziara yao ambapo leo wametembelea na kutoa elimu
katika kata ya Lyabukande pamoja na kata ya Lyamidati.
Pamoja na mambo mengine wamempongeza Rais Samia kwa
kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
ambapo wamesema fedha zilizoletwa na Rais Samia zimetekeleza katika
miradi mbalimbali kwenye sekta ya afya pamoja na elimu.
Pia wamempongeza Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed
Salum kwa maendeleo anayoyafanya katika Jimbo hilo.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe.
Zawadi Lufungulo Mwasha amesema ipo miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa
katika kata ya Lyabukande ikiwemo ujenzi wa madarasa pamoja na ujenzi wa
Zahanati.
“Nimpongeze
sana Rais wetu Mama Samia, amefanya mambo makubwa ya maendeleo kwa kipindi
kifupi tu mabadiliko ni makubwa yaani ndani ya Miaka mitatu hakuna mtu
aliyechangishwa michango kwenye ujenzi wa madarasa pia amekuwa akileta fedha za
miradi mbalimbali za maendeleo kwahiyo tunampongeza sana lakini pia hata mbunge
wetu wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum anasimamia jimbo letu vizuri sana tuendelee
kumuombea sana mbele za Mungu maana tukipoteza hii bahati sijui kama tutakuja
kuipata kwanza anaupendo na anahudumia wananchi wake bila upendeleo kwa sasa
hapa Lyamidati kuna ujenzi unaendeleo wa jengo wa ofisi ya Chama cha kata
ambayo ipo chini ya mheshimiwa mbunge kwahiyo niwaombe sana tuendelee kuwaunga
mkono viongozi hawa”.amesema Mhe. Zawadi
“Kuna
ukarabati wa madarasa ya shule ya msingi Lyabukande mradi huu fedha zimeletwa
na Rais Samia mpaka sasa mradi huu umefikia hatua ya upakaji rangi na vigae,
lakini pia kuna mradi wa ukarabati madarasa matatu kijiji cha Buzinza kata ya
Lyabukande fedha za mradi zimeletwa na Mama Samia na mradi umefikia hatua ya
upakaji rangi na vigae na alminiam”.
“Kuna
ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Ahamed Kimandaguli kutoka fedha za
jimbo ambapo mradi huu umefikia hatua ya usawa kufunga lenta, kuna ujenzi wa
madarasa manne na ofisi moja hapa Lyabukande fedha zinatoka kwenye mfuko wa
jimbo mradi huu umefikia hatua ya msingi tofari zipo”.
“Kuna
mradi wa Umeme REA kwenye kijiji cha Lyagiti, Mapingili, Mwamakala na Buzinza
fedha hizi zinatoka serikali kuu na mradi umefikia hatua ya ukamilishaji, lakini
pia kuna mradi wa Maji ya ziwa unaendelea ambao gharama yake ni Bilioni 1.4”.
“Upo
ujenzi wa Zahanati kijiji cha Mapingili ambapo boma tayari limekamilika, na
kuna ujenzi pia wa Zahanati kijiji cha Mwashagi kwa nguvu ya wananchi mradi
umefikia usawa wa msingi’.
“Miradi
mingine inayoendelea ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya msingi Ng’wanangi,
ujenzi wa choo cha mnada pamoja na ujenzi wa ofisi ya walimu Lyabukande
sekondari kwahiyo niwaombe sana wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi na
jumuiya zake tuendelea kuwaunga mkono viongozi wetu wote wanafanya vizuri
wanajitahidi sana kuleta maendeleo kwenye maeneo yetu”.
Katibu wa madiwani
viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anastazia Robart
Njile ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Tinde ameendelea kuwakumbusha
wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya zake kuwa kipaumbele wakati wa
kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura pamoja na daftari la makazi.
Katibu wa umoja
wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma amewasisitiza wanawake wa UWT kujiamini na
kuhakikisha wale wenye sifa wanachukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi katika vijiji na vitongoji
wakati utakapofika.
Pia amesisitiza wanachama kujisajili kwenye mfumo wa
kielekroniki ili kuendelea kuwa wanachama imara wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Kwa upande wake diwani wa viti maalum kata ya Tinde
Mhe. Helena Daud Mwanambuli ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wanawake kutoa
taarifa za ukatili wa kijinsia unaoendelea kufanyika katika familia, jamii na
maeneo mengine ili hatua zaidi za sheria ziweze kuchukuliwa kwa watuhumiwa.
Nao baadhi ya madiwani wengine wa viti maalum katika
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameendelea kumpongeza mbunge wa jimbo la
Solwa Mhe. Ahmed Salum kwa kazi anazozifanya ambazo zinalenga kuwaletea
maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Pia wameendelea kuwakumbusha wanawake na wanachama
wa CCM kuhakikisha wanakuwa kipaumbele katika hatua zote za uchaguzi wa
serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika badae Mwaka huu 2024 pamoja na
uchaguzi mkuu Mwaka 2025 ili waweze kumpigia kura mgombea wanayemhitaji kwa
haki na amani.
Wamewaomba wananchi kuendelea kuwaunga mkono
viongozi waliopo madarakani wakiwemo madiwani wa kata, mbunge wa jimbo la Solwa
pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa
katika shughuli za maendeleo.
Malengo ya ziara ya madiwani wa viti maalum
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni kuhamasisha wanawake na wanachama wote wa
CCM na jumuiya zake kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga
kura, kuhamasisha wanawake kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi, Usajili wa wanachama wa CCM na jumuiya zake pamoja na na
kukemea Ukatili wa kijinsia.
Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga leo Jumatano Julai 10,2024 wametembelea kata ya Lyabukande yenye
vijiji saba (7) ambavyo ni Mwamakasi, Lyabukande, Kimandaguli, Mapingili,
Lyangili, Buzinza pamoja na Mwashagi.
Lakini pia wametembelea kata ya Lyamidati ambayo ina
vijiji sita (6) ambavyo ni Ihagi, Kizungu, Mwabasa, Bukiligulu, Lyamidati pamoja
na Kadoto.
Baadhi ya wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya
zake wamewapongeza madiwani wa viti maalum kwa kufanya ziara hiyo ambapo
wameahidi kuzingatia yale yote ambayo wamekumbushwa iliwemo kuchua fomu za
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha akizungumza kwenye mkutano leo Julai 10,2024 katika kata ya Lyabukande.
Madiwa wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga baada ya kuwasili katika kata ya Lyabukande.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe.
Zawadi Lufungulo Mwasha akitoa zawadi kwa msanii ambaye ameimba wimbo maalum wa
CCM.
Katibu wa umoja
wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akizungumza kata ya Lyabukande Julai 10,2024.
Katibu wa umoja
wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akizungumza kata ya Lyabukande Julai 10,2024.
Katibu wa madiwani
viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti
maalum kata ya Tinde Mhe. Anastazia Robart Njile akizungumza kwenye mkutano huo
leo Julai 10,2024 katika kata ya Lyabukande.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha akizungumza kwenye mkutano huo leo Julai 10,2024 katika kata ya Lyabukande.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe.
Zawadi Lufungulo Mwasha akizungumza kwenye mkutano huo leo Julai 10,2024 katika
kata ya Lyabukande.
Katibu wa umoja
wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akizungumza kwenye mkutano huo leo Julai
10,2024 katika kata ya Lyamidati.
Katibu wa umoja
wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akizungumza kwenye mkutano huo leo Julai
10,2024 katika kata ya Lyamidati.
Katibu wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Tinde Mhe. Anastazia Robart Njile akizungumza kwenye mkutano huo leo Julai 10,2024 katika kata ya Lyamidati.
Katibu wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Tinde Mhe. Anastazia Robart Njile akizungumza kwenye mkutano huo leo Julai 10,2024 katika kata ya Lyamidati.