Na Mapuli Kitina Misalaba
Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga wamewahimiza wazazi, walezi na jamii kuwalea watoto katika maadili
mema na misingi inayozingatia mila na desturi za eneo husika ili kuepukana na
vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto.
Wameyasema
hayo leo Alhamisi Julai 11,2024 katika ziara yao kata ya Nyabusalu pamoja na
kata ya Iselamagazi ambapo wameendelea na ziara yao kwa lengo la kuhamasisha
wanawake na wanachama wote wa CCM na jumuiya zake kujitokeza kujiandikisha
kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kuhamasisha wanawake kujitokeza
kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Usajili wa wanachama wa
CCM na jumuiya zake pamoja na na kukemea Ukatili wa kijinsia.
Akizungumza Mwenyekiti wa madiwani viti maalum
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya
Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha amewasisitiza wazazi na walezi
kusimamia maadili kwa watoto huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea kukemea
mmomonyoko wa maadili.
“Ukatili
nimegundua kwamba ni malezi yanapungua yaani maadili yetu ya kitanzania
yamepolomoka sana motto usipomlea vizuri huyo ndiye atakuwa mbakaji, atakuwa
mlawiti, atakuwa shoga u nakuta motto amevaa mtepesho na wewe mama unaangalia
tu na wewe baba unaangalia tu ebu turudi kabisa kwenye maadili yetu tuwe wakali
watoto hawa tuwakemee kizazi chetu kimaharibika sana, hivyo hivyo viongozi wa
dini msaidie hili semeni makanisani semeni kwenye miskiti ili haya maadili
tuendane na mila zetu za kitanzania”.amesema Mhe. Zawadi
Aidha Mhe. Zawadi pamoja na mambo mengine ameendelea
kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungani wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe. Ahmed
Salum kwa kuendelea kuwahudumia wananchi kwa weledi katika utekelezaji wa
majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya
Chama cha Mapinduzi CCM.
Pia madiwani hao wamempongeza diwani wa kata ya
Lyabusalu kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo katika kata hiyo ikiwemo
mradi wa ujenzi wa Zahanati Lyabusalu, ujenzi wa Choo cha shule ya msingi
Lyabusalu B, ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Lyabusalu A, ujenzi wa
madarasa matatu katika shule ya msingi Bukamba pamoja na ujenzi wa nyumba ya
walimu shule ya msingi Mwajiji.
Pia wamempongeza kwa usimamizi mzuri katika ujenzi
wa darasa moja katika shule ya msingi Mwabagehu, ujenzi wa ofisi ya kijiji
Mwabagehu, ujenzi wa Zahanati kijiji cha Mwashilugula, ujenzi wa shule mpya ya
sekondari katika kijiji cha Mwasingu pamoja na ujenzi wa ofisi ya kata
Lyabusalu ambapo fedha za miradi zinatoka serikali kuu na zingine katika mfumo
wa jimbo.
Wakati huo huo madiwani wa viti maalum Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wao wamempongeza diwani wa kata
ya Iselamagazi Mhe. Isaack Sengerema kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo
inayotekelezwa ili kutatua kero na changamoto za wananchi.
“Tunampongeza
sana diwani wa kata ya Iselamagazi ipo miradi tumeitembelea tumeona hatua ni
nzuri hasa ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi
Iselamagazi ambao tumeona mradi umefikia hatua ya upauaji lakini pia kuna
ujenzi wa vyumba sita vya madarasa na matundu nane shule ya sekondari na
tumeambiwa mradi huu umefikia hatua ya mwisho”.
“Pia
kuna mradi wa uvutaji maji shule ya msingi Budushi tumeambiwa mradi huu
umekamilika kwahiyo tunampongeza sana diwani na mbunge wa jimbo letu la Solwa
lakini pia kuna mradi wa kituo cha Polisi Iselamagazi ambao tayari umekamilika
pamoja na ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Iselamagazi ambapo tumeambiwa boma
limepauliwa kwahiyo tunampongeza tena mbunge kwa kupambania upatikanaji wa
fedha za miradi pia tunampongeza diwani Isaack na Rais wetu Mama Samia kwa
kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo”.amesema
Mhe. Zawadi
Madiwani wa viti maalum katika ziara yao wameendelea kuwakumbusha wanawake na wanachama wa CCM kuhakikisha wanakuwa kipaumbele katika hatua zote za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika badae Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu Mwaka 2025 ikiwemo zoezi la kujiandikisha kwenye daftari ya balozi pamoja na daftari ya mpiga kura.
Katibu wa umoja
wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma ameendelea kuwasisitiza wanawake wa UWT
kujiamini na kuhakikisha wale wenye sifa wanachukua fomu kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi katika vijiji na
vitongoji wakati utakapofika .
Pia amesisitiza wanachama kujisajili kwenye mfumo wa
kielekroniki ili kuendelea kuwa wanachama imara wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Baadhi ya wanachama wa CCM na jumuiya zake
wamewapongeza madiwani wa viti maalum kwa kufanya ziara hiyo ambapo wameahidi
kuzingatia yale yote ambayo wamekumbushwa iliwemo kuchua fomu za kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi.
Pia wametumia nafasi hiyo kuiomba serikali
kuwachukua hatua kali za kisheria watu wanaobainika kufanya vitendo vya ukatili
ikiwemo upakaji na ulawiti kwa watoto.
Katibu wa umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akiwatambulisha madiwani baada ya kuwasili katika mkutano wao kata ya Lyamidati
.
Katibu wa umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akiwahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili kupata sifa ya kuwa mpiga kura.
Katibu wa umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akiwahimiza wanawake wa UWT kuwatambua haraka watu wenye wanawake wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe. Zawadi Lufungulo Mwasha akiwahimiza wanawake wote kujitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha katika daftari ya balozi na daftari la mpiga kura pia amesisitiza wanawake kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Katibu wa umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma akizungumza kwenye mkutano wa madiwani wa viti maalum katika kata ya Iselamagazi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Katibu wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Tinde Mhe. Anastazia Robart Njile akiwasisitiza wanawake kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bila uoga na kwamba wajiamini.
Katibu wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Tinde Mhe. Anastazia Robart Njile akiwasisitiza wanawake kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bila uoga na kwamba wajiamini.