Na Mapuli Kitina Misalaba
Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga Julai 9,2024 wameanza ziara yao kutembelea tarafa tatu za Halmashauri
hiyo kwa lengo la kuhamasisha wanawake na wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM
na jumuiya zake kushiriki vema katika hatua zote za uchaguzi wa serikali za
mitaa Mwaka huu 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inajumla ya kata
26 katika tarafa tatu ambapo leo madiwani wa viti maalum Halmashauri hiyo
wametembele na kutoa elimu hiyo kwenye kata ya Mwenge pamoja na kata ya Salawe zilizopo
tarafa ya Nindo na kwamba tarafa hiyo inajumla ya kata 12.
Katika kata ya Mwenge baadhi ya wanachama wa CCM na
jumuiya zake wamehudhuria kutoka kwenye vijiji mbalimbali ikiwemo Ipango,
Mwenge, Zunzuli, Ihimbili, Mongozo pamoja na Ipango.
Kata ya Salawe imehudhuriwa na wanachama wa CCM na
jumuiya zake kutoka vijiji vitano ikiwemo Azimio, Amani, Buduhe, Nzoza pamoja
na kijiji cha Songambele.
Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyabukande Mhe.
Zawadi Lufungulo amehimiza wananchi wote kushiriki kikamilifu katika zoezi la
uandikishaji wa daftari la mpiga kura pamoja na daftari ya makazi ili kuwa na
sifa za kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa
kufanyika badae Mwaka huu 2024.
Pia amewasisitiza wanawake wa UWT kujiamini na
kuhakikisha wale wenye sifa wanachukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi ikiwemo nafasi ya wenyeviti wa
vijiji, mitaa pamoja na balozi.
Katibu wa madiwani
viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anastazia Robart
Njile amezihimiza jumuiya za CCM ikiwemo UWT kuanza kuwatambua na kuwashawishi
watu wenye sifa za uongozi wahakikishe wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali
baada ya zoezi hilo kuanza.
Katibu wa umoja
wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma ametaja baadhi ya sifa za mtu anayetaka kugombea nafasi
ya uongozi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.
“Sifa
ya kwanza unatakiwa uwe mwanachama wa CCM hii ndiyo sifa ya kwanza yaw ewe
kugombea katika Chama chetu cha CCM vile vile uwe mkweli na mwenye maadili mema
usife mlevi kingine awe mstari wa mbele kuhudhuria vikao vya chama kwa mujibu
wa katiba, awe anakubalika kwa dhati na watu kwahiyo tukachague viongozi
wanaokubalika kwenye jamii, awe mpenda maendeleo na mbunifu, awe mwenye kuona
mbali na aweze kusoma mazingira awe na maamuzi ya bila kuyumbishwa na mtu yoyote
asiwe mwenye makundi ya kuchochea migogoro sifa nyingine mgombea wa CCM awe
anajua kusoma na kuandika”.amesema Dodoma
Kwa upande wake diwani wa viti maalum kata ya Tinde
Mhe. Helena Daud Mwanambuli pamoja na mambo mengine amekemea rushwa na ngono huku
akiwasisitiza wanawake kutoa taarifa za watu watakaoomba rushwa ya ngono katika
kipindi cha uchaguzi.
Nao baadhi ya madiwani wengine wa viti maalum katika
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamewaomba wananchi kuendelea kuwaunga mkono
viongozi waliopo madarakani wakiwemo madiwani wa kata, mbunge wa jimbo la Solwa
pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa
katika shughuli za maendeleo.
Malengo ya ziara hiyo ni kuhamasisha wanawake na
wanachama wote wa CCM kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura, kuhamasisha wanawake kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali
za uongozi, Usajili wa wanachama wa CCM na jumuiya zake pamoja na na kukemea Ukatili
wa kijinsia.
Baadhi ya wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya
zake wamewapongeza madiwani wa viti maalum kwa kufanya ziara hiyo ambapo
wameahidi kuzingatia yale yote ambayo wamekumbushwa iliwemo kuchua fomu za kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi.
Katibu wa umoja wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini
Bi. Magdalena Dodoma akitaja sifa za kiongozi.