MADIWANI WAN'GAKA WAKANDARASI KUCHELEWA KUKAMILISHA MIRADI NDANI YA MUDA WA MKATABA

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaBaraza la Madiwani Manisipaa ya Shinyanga limewataka wakanda wanaotekeleza miradi ya Barabara za Mijini na Vijijini TARURA kukamilisha ujenzi wa Miundombinu za barabara ndani ya mukataba. 
Waheshimiwa Madiwani wamebainisha hayo leo Julai 30.kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kupokea taarifa mbalimbali kutoka Tasisi za Serikali pamoja na kamati za kudumu ambapo wamesema kumekuwepo na ucheleweshwaji kukamilika kwa miundombinuu ya barabara za mijini na vijijini kutoka kwa Wakandarasi hao. " Kunakivuko ambacho kinatoka Mwamala Masekelo kuelekea katika kata ya Ibinzamata, Kitangili pamoja na Kizumbi kivuko hiki ni chamuhimu sana kwasababu kinaunganganiisha kata hizo, Mwaka 2015 kunawanafunzi wawili walifariki kutokana na kivuko hicho, tulipata barua tarehe 26/06 /2024 ya kuanza kutengeneza kivuko hicho lakini mpaka sasa hakuna chochote kinaendelea". Amesema Mhe, Piter Koliba. Diwanni wa kata ya Masekelo. "Kamkandarasi anaitwa UK anaetekeleza mradi kata ya Kizumbi Mkataba umeisha tangu tarehe 29/07/2024 mpaka sasa kazi haijaisha sasa kunajiagani nyinggine ya kutusaiddia ili wananchi hao wapate huduma ya barabara kwa haraka? "Amesema Mhe, Ruben Kitinya Diwani wa kata ya Kizumbi. Akitoa ufafanuzi wa kuchelewakwa kukamilika kwa barabara hizo Kaimu Meneja TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Yohana William amesema kwa  mwaka wa fedha 2023/2024 walitengewa Shilingi bilioni 2.9 lakini pesa zilizofika na kufanya kazi ni milioni miatisa tu 9,000,000/=Naye mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe, Elias Masumbuko amesema suala la kutokamilika kwa barabara hizo lipo nje ya wakala wa barabara Mijini na Vijijini Tanzania TARURA kwa sababu wakandarasi hao hawajalipwa stahiki zao"Kama fedha zingekuwepo hoja zote hizi zisingekuwepo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wakandarasi wanadai stahiki zao, hivyo tunatakiwa tuwapongeze TARURA kufanya kazi katika mazingira ya namna hiyo". Amesema Msitahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe, Masumbuko.Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe, Elias Masumbuko akizungumza kwenye baraza hilo leo Julai 30,2024.Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza kwenye baraza la madiwani leo Julai 30,2024.Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Mhe. Anord Makombe akitoa salamu zake za chama kwenye baraza hilo leo Julai 30,2024.Katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Kaimu Meneja TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Yohana William akitoa ufafanuzi wa kuchelewakwa kukamilika kwa barabara hizo.

 

Previous Post Next Post