Mbinu zenye kuleta mafanikio kwa haraka

 


Kuna wakati unahitaji mambo mengi ya kuyafahamu ili uweze kufanikiwa kimaisha.  Hivyo kwa kila jambo ambalo unataka likuletee mafanikio ni lazima ujue ni kwa namna gani litakuletea mafanikio.
Watu wengi tunaingia kufanya mambo ya kimafanikio kwa njia za kawaida sana. Kitu hicho ambacho kinatufanya kila siku tubaki mahali pamoja kila siku na kushindwa kusonga mbele kimafanikio. Lakini katika makala haya nitakuibia siri mbili ambazo ukizifuata zitakufanya uweze kufanikiwa.

Zifuatavyo ni njia mbili zenye kukuletea mafanikio;
Jambo la kwanza Jifunze  vipya kila siku.
Kwa asilimia kubwa watu wengi hatupendi kujifunza vitu vipya hasa kwa staili ya kusoma vitabu, magezeti, majarida na vitu vingine ambavyo vitatufanya vituongezee maarifa na ujuzi. Ngoja nikupe stori mmoja ambayo iliwahi kumpata rafiki yangu wa karibu. Rafiki ambaye nilisoma kipindi cha nyuma.  Mnamo miaka kadhaa baada ya kumaliza masoma alipata ajira, baada ya hapo aliweza kupata jiko yaani (mke) ambaye walipendana sana,
Siku moja katika harusi yake alizawadia zawadi ya kitabu cha Mungu (Biblia) na rafiki yake wa karibu ambayo ndani biblia hiyo ilikuwa na cheki yenye thamani ya fedha nyingi. Kwa kuwa  rafiki yangu huyo hakuwa na tabia ya kusoma vitabu na hajawahi kuisoma biblia ile ambayo alipewa hivyo  hakuiona  cheki ile, kwa hiyo cheki ile aliisha muda wake bila yeye kujua.

Mwisho wa siku Yule aliyempa biblia ile alikuja kumuonesha kwamba katikati  ya biblia alimuzawadia  zawadi ya cheki pia. Kwa kuwa Yule rafiki yangu hakuwa na kawaida kujisomea kitabu. Hivyo alikosa zawadi ya cheki yenye thamani kubwa ya fedaha nyingi.  Kisa hiki kinatuonesha ni  jinsi gani watu tulivo kuwa hatupendi kujifunza mambo mbalimbali kwa njia ya kusoma.

Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kuwa tayari  kujifunza vitu vipya kila siku. Kiuhalisia ni kwamba  watu wengi wanaamini kujifunza  ni mpaka uingine darasani kitu ambacho sio kweli hata kidogo.

Mtu anaweza  Kujifunza  kwa kutazama vitu au shughuli na jinsi gani watu wengine wanafanya.
Kuna wakati mwingine unahitaji muda wa ziada, kila siku uweze kujifunza vitu hivyo. Kama kweli unahitaji mafanikio weka ratiba kila siku ya kujifunza vitu vipya vitakavyokufanya uongeze thamani kwa kile unachotaraji kiweze kutimiza malengo yako.

 Kuna swali dogo huwa najiuliza hivi wasanii wa nyimbo wangekuwa wanasilisha kazi zao za kwa mashabiki zao kwa njia ya maandishi ya kusoma ni wasanii wangapi tungekuwa tunawajua?   uhalisia  wa jambo hilo ni kwamba ni wasanii wachache mno ambao tungekuwa tunawafahamu kwa sababu wengi wetu hatupendi kusoma vitabu na vitu vingine. Ewe mdau wa makala haya jaribu kuhakikisha ya kwamba kila wakati unajifunza vitu vipya. Jiulize ni kitu gani ambacho umekipa kwa kila siku kwa njia ya kujifunza?

Jambo la pili jiulize maswali kwa kila jambo.
Kwa msaka maendeleo na mafanikio kuwa na  tabia hii ya kujiuliza maswali ni kawaida. Kama wewe huna utaratibu huu wa kujiuliza maswali inawezekana kwa asilimia kubwa ikawa ndo sababu ya kubaki hapo ulipo. Ila kama kama unataka kufanikiwa ni lazima ujilize maswali. Kama wewe ni mfanyabiashara, mkulima, mwanafunzi, fundi au kazi yeyote ile jitahidi kuwa na uratibu wa kujiuliza maswali mfano. Nifanye nini ili niweze kufanikawa kwa kuongeza wateja, je nifanye nini ili kufaulu katika masomo yangu na maswali mengine mengi kama hayo.

Wakati unajenga utaratibu huo wa kujiuliza maswali mwenyewe hakikisha kwa kila swali ambalo unajiuliza unapata majibu ya maswali hayo. Nafikiri mpaka hapo utakuwa umenielewa vizuri.

Kuna msanii mmoja hapa nchini aliwahi kuimba ya kwamba utaratibu wake ni kuuliza why, hivyo hata wewe jijengee utaribu huo utaona ni kwa jinsi gani utavyofanikiwa. Niliyoyasema hapo juu yote ni uongo kama utashindwa kuchukua hatua, yatakuwa ukweli endapo utaamua kuyaweka katika matendo.

Asante sana kwa kuendelea kujifunza kupitia mtandao wa  Dira ya mafanikio. Mpaka kufikia hapo sina la ziada tukutane tena katika makala ijayo.
Previous Post Next Post