MBUNGE IDDI ASIKITISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI AMTAKA MKURUGENZI AENDE AKAJIONE UBADHILIFU WA FEDHA


Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Khamis Katimba kutembelea na kukagua miradi ya kimkakati iliyopo kwenye halmashauri hiyo na kuchukua hatua za kuhakikisha inakamilika katika ubora ambao umepangwa na serikali.

Mbunge Iddi ametoa kauli hiyo kutokana na malalamiko ya wananchi wa Kijiji cha Kabondo Kata ya Mwanase ,ambao wamedai pamoja na kila kaya kuchangia kiasi cha sh,elfu 40 na serikali kuu kutoa zaidi ya Milion Hamsini mradi wa ujenzi wa Zahanati umekuwa ukisua sua kwa muda mrefu na kushindwa kukamilika hali ambayo imepelekea kwa sasa jingo kuanza kubomoka kutokana na kushindwa kuendelezwa.

“Mbunge nataka kujua sisi wananchi tumechangishwa kila kaya elfu 40 lakini ,hii Zahanati wajumbe wanaoteuliwa kusimamia niwakina nani ujenzi huu aujawai kukamilika tangu umeanza unamiaka miwili ninavyokumbuka sasa ninamashaka  kuna dalili za upigaji aiwezekani mradi mkubwa kama huu kuchukua miaka yote hiyo bila kukamilika na cha kushangaza ukifika pale tayari jengo limeanza kutokea na nyufa kubwa”Alisema Salum Masasila Changalawe.

Kufuatia madai hayo Mbunge Iddi akamtaka msimamizi wa mradi huo ambaye ni mganga mfawidhi  Zahanati ya Mwanase Don Leornad ,amesema fedha zote ziliingia kwa kupitia kwenye akaunti ya zahanati ya Mwanase kiasi cha million hamsini na awamu ya pili walipokea kiasi cha milioni kumi ambapo waliona busara ni kushirkisha wajumbe wa Mwanase na wa Kijiji cha Kabondo.

“Ni kweli kuna mipasuka imetokea lakini wataalamu walifika wakasema mzigo ambao umeupata kwa sasa kutokana na kusimama kwa muda mrefu jengo limeanza kushuka upya ,lakini hata makisio ya kutekeleza mradi wa Zahanati ya Kabondo aijakisiwa kwani kawaida ilitakiwa iwe  zaidi ya Milioni themanini bado hazijafikiwa”Don Leornad Msimamizi wa ujenzi.

Hata hivyo Mbunge Iddi ameonesha kutokulizishwa na majibu ya msimamizi wa mradi huo kutokana na kuchukua muda na kuonesha kuwa umetekelezwa  bila ya kufuatiliwa na kiongozi yoyote wa Halmashauri.

“Nimeuombe Mkurugenzi miradi hii serikali inatoa fedha nyingi sana sioni sababu ya yeye kushindwa kufuatilia na kufanya ukaguzi kwenye hii miradi nimuombe aje afuatilie kwenye jimbo zima tulikuwa na Zahanati 34 hazijakamilika ,na hapa nilileta milioni hamsini ,Hapa na Mwakima cha kushangaza wengine wamekamilisha hapa kunanini  au kuna nani ambaye amekuwa akitafuna fedha au kuna mashetani tuwaombe watu waje wafanye maombi inasikitisha sanaa “Alisema Iddi Kassim Iddi Mbunge wa Msalala.

“Naomba niwahakikishie wananchi wnagu Mimi Mbunge wenu mmeniamini mkanichagua niwatumikie na kuwakilisha kero zenu niwahakikishie sitakuwa chanzo au sababu ya kuwakwamisha kufikia ndoto za maendeleo ambazo mnaziitaji nitashughulika na yeyote ambaye atacheza na mali ya umma” Alisema Iddi Kassim Iddi Mbunge wa Msalala.

MWISHO..

 

Previous Post Next Post