MENEJIMENTI YA SHUWASA IKIONGOZWA NA MHANDISI KATOPOLA YATEMBELEA KATA YA NDALA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WATEJA


Menejimenti ya SHUWASA ikiongozwa 

na Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Yusuph Katopola Leo Julai 12. 2024 imetembelea kata ya Ndala kwa lengo la kusikiliza changamoto zitokanazo na huduma ya Majisafi, elimu kuhusiana na huduma za SHUWASA pamoja na kuhamasisha wateja wenye madeni kulipa Ankara zao za maji.

 Zoezi hili ni endelevu na litafanyika kwa kata zote za Manispaa ya Shinyanga na maeneo ya pembeni (Tinde, Didia na Iselamgazi) yanayohudumiwa na Mamlaka hiyo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola amesema zoezi hili litasaidia kujua changamoto zilizopo na kuboresha zaidi utoaji wa huduma katika maeneo yote yanayohudumiwa na Mamlaka hiyo.

 Vilevile amesema ni njia mojawapo ya kujenga mahusiano mazuri na ya karibu na wateja pamoja na jamii kwa ujumla.


 

Previous Post Next Post