MHE. NDEJEMBI APONGEZA MAFANIKIO NSSF

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametembelea banda la NSSF katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu kama SabaSaba na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutokana na kupata mafanikio mbalimbali katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Aidha, Mhe. Ndejembi amejionea NSSF inavyotoa elimu ya hifadhi ya jamii, usajili wa wananchi walio katika sekta isiyo rasmi, mifumo ya TEHAMA, mapambano dhidi ya rushwa, miradi ya uwekezaji na huduma za NSSF kidijitali.

Previous Post Next Post