MICHAEL AHUKUMIWA MIAKA 30 KWA KUMBAKA BINTI YAKE WA KAMBO MWANZA


Mkazi wa  Nyambiti, Ngudu wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza Michael John Christopher kwa jina maalufu Omoro amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka binti yake wa kambo (14).

awali mshtakiwa alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kwimba terehe 9.04.2024 na kusomewa shitaka moja la kubaka na Mkaguzi wa Polisi Juma Kiparo mbele ya Hakim Mkazi Mwandamizi John Chai Jagadi ambapo mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na kesi iliahirishwa hadi tarehe 24.04.2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali (PH).

kwa mujibu wa hati ya mashitaka mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 20.12.2023 hadi tarehe 25.03.2024 huko katika mtaa wa Majengo Nyambiti ndani ya wilaya ya Kwimba na mkoa wa Mwanza.

Kiparo amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1)(2)(e) na 131 (1) vyote vya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya sheria marejeo ya mwaka 2022.

Mshitakiwa ambaye ni baba wa kambo wa Mhanga ambapo mama wa Mhanga huyo alifariki mwaka 2020 na kumuacha binti huyo mikononi mwa baba huyo.

Mshitakiwa alianza kufanya mapenzi na binti huyo tangu mwaka 2022 wakiwa wilaya ya Lolya mkoa wa Mara na hadi walipo hamia mkoa wa Mwanza tarehe 20.12. 2023.

Baada ya kuhamia mkoa wa Mwanza mtuhumiwa aliendelea kufanya mapenzi na binti huyo wa miaka 14 hadi ilipofika tarehe 25 .03.2024 ambapo binti alikataa kufanya mapenzi na baba yake wa kambo baada ya kushauriwa kufanya hivyo na mama yeke mkubwa na kupelekea baba huyo kumshushushia kipigo binti huyo kwakile alichodai kumnyimba unyumba.

Kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri mbele ya mahakama hiyo pasi na kuacha shaka umefanikisha mshtakiwa kuhukumiwa kifungo hicho.

Hata hivyo mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea alisema kwamba alikuwa akilala chumba kimoja na binti huyo baada chumba kingine kukirudisha kwa mwenye nyumba kwa kushindwa kulipa kodi ya chumba cha pili  ambapo hakimu alitupilia mbali ombi hilo na kumhukumu kwenda jela miaka 30 ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Previous Post Next Post