Mgeni rasmi katika tamasha la utamaduni wa Msukuma Shinyanga, Naibu katibu mkuu wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Suleiman Serera akimkabidhi cheti cha pongezi Mapuli Kitina Misalaba ambaye ndiye Mkurugenzi wa Misalaba Media na kwamba cheti hicho kimetolewa na Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK).
Misalaba Media ni chombo cha habari, kinachakata na kusambaza habari mbalimbali mtandaoni na kwamba cheti cha pongezi kinafuatilia baada ya kuripo habari za tamasha la utamaduni wa wa Msukuma ambalo limeandaliwa na Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK).
Tamasha hilo hufanyika kila Mwaka katika viwanja cha shule ya msingi Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga ambapo Mwaka huu 2024 limefanyika kwa siku mbili na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mila na desturi pamoja na viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, kaimu mkurugenzi maendeleo ya utamaduni kutoka Wizara ya utamaduni, sanaa na Michezo.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo kwa Mwaka huu ni Naibu katibu mkuu wizara ya utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Suleiman Serera.
“SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3, LEJIGUKULU LYA NZENGO”