MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ANAMRINGI MACHA AWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUDUMISHA AMANI, KUWAENZI MASHUJAA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, amewaomba wananchi Mkoani Shinyanga  kuendelea kudumisha Amani umoja na mshikamano  ikiwa ni ishara ya kuwaenzi mashujaa waliopigania Uhuru wa taifa la Tanzania.

Ameyasema hayo leo  kwenye maadhimisho ya kumbukumbu siku ya mashujaa kitaifa  yaliyofanyika kwenye mnara wa mashujaa uliopo katika eneo la mazingira centre Mjini Shinyanga,ambapo amesisitiza kuendelea kuenzi mchango wa viongozi hao ambao walijitoa mhanga kupigania taifa la Tanzania kwa moyo wa uzalendo

RC Macha amesema Mashujaa hao walipigania Uhuru wa Taifa hili kwa kutumia silaha za Jadi ambapo  amewasisitiza  watanzania kuendelea kuwaenzi Mashujaa hao kwa kudumisha amani ya nchi ikiwa ni pamoja na kuwapongeza marais ambao wameongeza taifa hili.

Misalaba Media imezungumza na baadhi ya viongozi wa Dini na kimila ambao wamesema wameendelea kuhamasisha Amani kupitiia mahubiri katika nyumba za ibada  na mikutano ya hadhara kwenye majukwaa.

Wananchi Mkoani Shinyanga leo wameungana na watanzania wenzao Nchini kote kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mashujaa kitaifa ambayo hufanyika Julai 25, ya kila Mwaka.

TAZAMA VIDEO.


Previous Post Next Post