MR. BLACK KATIKA MKUTANO WA VIJANA WAWEKEZAJI NAIROBI KENYA

 Mr. BLACK (Peter Alex Frank) ndani ya ubalozi wa Tanzania nchini Kenya kwa ziara maalumu ya miradi ya kielimu na ujasiliamali kwa vijana. 

Mr. Black ambae pia ni mkurugenzi wa BSL SCHOOLS na THE BSL INVESTMENTS yuko Nairobi Kenya akiwa mmoja kati ya watoa mada wa kimataifa katika Kongamano la Vijana la ujasiriamali katika vyuo vya Nairobi Kenya.

 Kongamano hilo limepewa jina la Annual Youth Entreprenuership Summit linaloratibiwa na taasisi ya National Youth Caucus of Kenya. 

Kongamano limebeba vijana mashuhuri na wawekezaji vijana katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Kutoka Tanzania Mr. Black amekua mwakilishi. Hii ni chachu zaidi kwa ukuzaji maarifa, uchumi na mahusiano ya kitaifa.

Mr. Black pia ameendelea kuwakaribisha vijana kukua katika uwekezaji kimataifa na wasilisho lake kupitia kongamano hili limetoa hamasa kubwa zaidi kwa vijana washiriki wote.

Previous Post Next Post