MTEMI WA BUSIYA CHIEF EDWARD MAKWAIA ATEMBELEA KITUO CHA URASIMISHAJI, UWEKEZAJI NA UENDESHAJI BIASHARA MANISPAA YA SHINYANGA

Mtemi wa Busiya, Chief Edward Makwaia ameambatana na waratibu wake wa shughuli za Utemi kutembelea Kituo cha Urasimishaji Uwekezaji na Uendelezaji Biashara katika Manispaa ya Shinyanga.

Hii ni baada ya kumaliza Tamasha la Sanjo ya Busiya kwa mafanikio makubwa. Kama wanachama wa TCCIA, wameona ni vema kufika na kuona kituo cha taarifa za Utalii kilichoko hapo mnara wa Voda, mjini Shinyanga.

Mtemi ameshukuru kwa kupatikana kwa kituo cha taarifa za Utalii na kuahidi kuleta bidhaa na huduma mbalimbali katika Kituo hicho ili kuutangaza Utamaduni wa msukuma ndani ya mkoa wa Shinyanga lakini pia kwa wale watakaopita kutembelea Kituo hicho.

Nae Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa, Ndugu Hatib Mgeja amepongeza juhudi zinazofanywa na Utemi wa Busiya katika kudumisha Utamaduni na ameahidi kuendeleza mashirikiano kati ya TCCIA Mkoa na Utemi wa Busiya kwenye sekta ya Utalii.

Katibu wa TCCIA Mkoa Mama Marcelina Saulo ameshukuru kwa ugeni wa Mtemi na kwamba watajitahidi kutafuta wadau wa utamaduni na wale wa Utalii kama Balozi mbalimbali kuja kuongeza nguvu katika kuboresha shughuli za utamaduni zitakazovutia Utalii zaidi hapa mkoani Shinyanga.


Mtemi wa Busiya, Chief Edward Makwaia na  waratibu wake wa shughuli za Utemi wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Kituo cha Urasimishaji,  Uwekezaji na Uendelezaji Biashara  Manispaa ya Shinyanga.
Mtemi wa Busiya, Chief Edward Makwaia wa kwanza upande wa kushoto.








Mtemi wa Busiya, Chief Edward Makwaia na waratibu wake wa shughuli za Utemi wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Kituo cha Urasimishaji, Uwekezaji na Uendelezaji Biashara Manispaa ya Shinyanga.





Previous Post Next Post