Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Hamis
Mwinjuma (Mwana FA), amempongeza Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe.
Paschal Patrobas Katambi kwa kuibua vipaji vya vijana kupitia ligi aliyoiandaa
kwa kuwa mpira ni ajira.
Mwijuma ametoa pongezi hizo wakati akizindua Rasmi
Ligi ya Dr. Samia/ Katambi Cup ambayo imelenga kuibua vipaji vya vijana,na
itashirikisha timu 32 za mpira wa miguu katika Mkoa wa Shinyanga.
Ligi hiyo imezinduliwa katika viwanja vya Jasco
vilivyopo Ngokolo, na kucheza michezo mbalimbali ikiwamo ya kuvuta
kamba,kukimbiza kuku,kuchoma nyama ambapo washindi waliibuka na zawadi, na timu
hizo 32 za mpira wa miguu zitatimua vumbi katika viwanja mbalimbali.
Naibu Waziri huyo Mhe. Mwijuma amewaomba wananchi wa Shinyanga kwamba wasije
jaribu kumpoteza mbunge huyo bali wanapaswa kumlinda na kumpigania kwa nguvu
zote ili aendelee kuwa mbunge wao na kuwaletea maendeleo.
“Rais
wetu Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan anapenda michezo hivyo Katambi
kuanzisha ligi hii ni kumuunga Mkono Rais katika kukuza michezo hapa nchini na
kutoa ajira kwa vijana,”amesema Mwinjuma.
“Katambi
ni Mbunge ambaye anachapa kazi, ni mtu mwenye maarifa makubwa sana, hata Rais
Samia ana mwamini katika kumsaidia kazi na kuwatumikia Watanzania wote,hivyo
anapaswa kulindwa na kupiganiwa Wabunge kama hawa wapo wachache msije
kumpoteza,”ameongeza.
Zawadi ambazo watapewa washindi kwenye ligi hiyo, mshindi
wa kwanza wa mpira wa miguu, anapewa kiasi cha Shilingi milioni 6 pamoja na
kombe, mpira na jezi, mshindi wa pili atapewa Shilingi milioni 3, kombe,mpira
na jezi, huku mshindi wa tatu atapewa Sh.milioni moja,mpira na jezi.