PICHA MBALIMBALI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ANAMRINGI MACHA WAKATI AKIKAGUA MABANDA KWENYE AFYA CODE CLINIC

Mkuu wa mkoa wa shinyanga Mhe. Annamringi Macha amewaomba wananchi wa mkoa wa shinyanga  kuchangia damu kwenye Benki ya damu salama ili kusaidia watu wenye uhitaji wa huduma hiyo.

Ameyasema hayo leo wakati  akizindua  kampeni  ya “AFYA CODE CLINIC” 2024  inayoendelea katika  uwanja wa CCM kambarage  Mjini   Shinyanga ambapo huduma mbalimbali za Uchunguzi,matibabu,Chanjo,tohara kwa wanaume na Uchangiaji wa wa damu vinaendelea kutolewa kwa wananchi, sanjari na elimu kuhusu masuala ya kiafya

RC Annamringi Macha amesema uchangiaji wa damu umelenga kuwa na akiba kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wenye uhitaji wakiwemo wagonjwa,mama wajawazito pamoja na majeruhi wa ajali

Amewaomba wananchi kujiunga na bima ya Afya NHIF na chf iliyoboreshwa ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za afya zilizoboreshwa kwa wakati wote

Kwa upande wake Mganga Mkuu   wa Mkoa wa Shinyanga   Dkt Yudaz Ndungile amesema kampeini ya Afya Code Clinic imelenga kutoa huduma bure kwa wananchi wenye changamoto za kiafya ambapo madaktari bingwa, wataalam na wadau mbalimbali wa masuala ya afya wanaendelea kuwahudumia wananchi.

Previous Post Next Post