RC BABU ATOA AGIZO KWA WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA HALMASHAURI ZOTE MKOANI KILIMANJARO


Zawad  Antony, SAME MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ametoa agizo kwa wakuu wa idara na vitengo wa  halmashauri zote mkoani huko kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kudhibiti hoja za mdhibiti mkuu wa serikali badala la kuwaachia mweka hazina na Mkaguzi wa ndani pekee.

Babu alitoa  agizo hilo  jana  wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kujadili hoja tisa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka 2023.

"Hawa sio wenye hoja peke yao, nyie wakuu wa idara  na wakuu wa vitengo hili ni jukumu lenu wote,  mkiwaachia peke yao hawatawezi kufanya hiyo kazi,naomba  suala la  hili lizikatiwe katika  kumaliza au kupunguza hoja,"alisema 

Alisema kwa kufanya hivyo ni kukabiliana na hoja ambazo huletea halimashauri doa huku akiwataka  kuhakikisha mkaguzi wa Hesabu za Serikali anapata vitendea kazi ikiwemo mafuta ya gari kwa wakati na kwa haraka. 

Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliipongeza halmashauri hiyo kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo pamoja na kupunguza hoja za Mkaguzi kutoka 40 hadi kufikia hoja 9.

"Ila mnavyanzo vingi sana vya mapato,  tunaomba  mnendelee kuwa wabunifu na kuongeza bajet,"alisema RC Babu

Aidha Katibu tawala wa msaidizi wa mkoa, usimamizi ufuatiliaji na ukaguzi miradi Ponceano Kilumbi alizitaka kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni hasa kwa mikopo ya wanawake, vijana na wa watu wenye ulemavu.

Aidha mwenyekiti wa halmashauri  ya wilaya ya Same, Yusti  Mapande, aliahidi ushirikiano wa baraza pamoja na watendaji katika kumaliza  hoja au kuzimaliza kabisa.

"Ila tunaomba zile hoja za  kisera zibaki kwa ngazi ya mkoa  ili waweze kuziandikia kwa ngazi ya wizara na kupatiwa majibu,"alisema Mapande.

Previous Post Next Post