Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (kushoto mwenye shati jeupe) akiwa katika Banda la Benki ya CRDD leo Julai 25,2024 wakati akifungua rasmi Kampeni ya Afya Code Clinic ya matibabu bure kwa wananchi inayofanyika katika viwanja vya CCM Kambarage Mjini Shinyanga ambapo Benki ya CRDB ni Mdhamini Mkuu wa Kampeni hiyo.
Mapuli Misalaba na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Benki ya CRDB imeshiriki kama Mdhamini Mkuu kwenye Kampeni ya Afya Code Clinic ya matibabu bure kwa wananchi mkoani Shinyanga inayofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga ikiendeshwa na Jambo Group kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amesema Benki ya CRDB inashiriki Maonesho ya Afya Code Clinic kwa kwa kutoa elimu ya fedha kwa wananchi mbalimbali waliofika katika Uwanja wa CCM Kambarage ambapo amewasisitiza kuweka akiba ili ikitokea dharura ya kuumwa mtu awe na akiba ya kujitibu yeye ama mwanafamilia.
"Benki ya CRDB tumeshiriki kama wadhamini wakuu wa Afya Code Clinic ambapo hii inaendelea kudumisha mahusiano kati ya CRDB na Jambo Group. Kupitia Afya Code Clinic CRDB tunaendeleza kauli mbiu yetu ya ULIPO TUPO", amesema Wagana.
"Tupo hapa kwa ajili ya kuwapa wadau elimu ya kujiwekea akiba, tunawafungulia akaunti mbalimbali. Tunazo akaunti za makundi mbalimbali ambapo zingine hazina makato ya mwezi na zingine hazina makato wakati wa kutoa mfano Akaunti HODARI kwa wafanyabiashara.
Kupitia Afya Code Clinic tunawapa wananchi elimu namna ya kujiwekea akiba kwa kile wanachokipata na endapo ikitokea dharura unaumwa basi unatumia fedha uliyojiwekea akiba kwa ajili ya matibabu. CRDB imekuwa mdau mkubwa wa masuala ya afya kupitia CRDB Marathon lengo kubwa ni kupata fedha kwa ajili ya kusaidia matibabu kwa wahitaji mbalimbali na tumekuwa tukitoa bima za afya",ameongeza Wagana.
Akiwa katika Banda la CRDB, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameipongeza Benki ya CRDB kwa ushirikiano na huduma mbalimbali inazotoa huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Benki hiyo.
"Tunawashukuru sana, hatuna sababu yoyote ya kuwa na mashaka ya kuitaja CRDB ni benki kubwa nchini, ni benki inayofahamika, benki ambayo inatoa huduma, benki ambayo ni mdau wa wananchi na serikali katika maendeleo ya nchi hii kiuchumi, kwa hiyo tunawapongeza sana",amesema Mhe. Macha
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akimwelezea Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) kuhusu huduma zinazotolewa katika benki ya CRDB
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akimwelezea Diwani wa Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulam Hafeez Mukadam (kulia) kuhusu huduma zinazotolewa katika benki ya CRDB.