TET, ZJNU ZAINGIA MAKUBALIANO KUIMARISHA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI WA MASOMO YA SAYANSI

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imesaini makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University (ZJNU) cha nchini China kwa lengo la kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi.

Akizungumza leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba, alisema ushirikianao huo utasaidia kuanzisha kituo cha Elimu ya Sayansi na Kidiijitali na kuifanya TET kuwa kituo cha mafunzo cha kikanda katika masomo ya sayansi.

Pia alibainisha shughuli mbalimbali zitakazotekelezwa kutokana na mkataba huo ikiwemo kuimarisha uwezo wa wakuza mitaala, walimu mahiri na wakufunzi wa masomo ya sayansi kupitia kozi fupi. 

“Kuimarisha uwezo wa wakuza mitaala kupitia kozi za muda mrefu kupitia fursa za mafunzo ya shahada ya uzamili na uzamivu. Kufanya shughuli za kubadilishana maarifa kwa kufanya tafiti.

“Kushirikiana katika kuandaa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu vya kiada, miongozo, moduli na matini zenye maudhui ya kieletroniki,” alisema Dk. Aneth.

Aliongeza kuwa kutakuwa na ziara za kimasomo za kubadilishana wataaluma kutoka TET na ZJNU ili kupeana uzoefu na ujuzi kwenye maeneo mbalimbali ya kielimu hasa elimu ya sayansi na kidijitali.

Eneo lingine ni kuweko kwa ziara za wanafunzi, wanaotaka kufanya programu fupi na kushirikiana katika kuandaa mikutano na makongamno ya kielimu ya kimataifa itakayofanyika nchini China au Tanzania kila mwaka.  

Mkuu wa Chuo cha ZJNU, Prof. Huang Xiao, alisema ushirikiano huo unasisitiza dhamira yao ya pamoja ya kuendeleza elimu na kukuza uvumbuzi kuhusu elimu ya kidijitali. Na kwamba wana historia yenye manufaa ya ushirikiano na taasisi za elimu Afrika.

Alisema katika chuo hicho wamekuwa wakitekeleza mkakati wa utandawazi na kuanzisha mawasiliano ya kina na vyuo vikuu kote ulimwenguni, kama Chuo Kikuu cha Kansas nchini Marekani na cha Malkia Uingereza.

“Leo, tunarasimisha ushirikiano wetu na TET kwa kutia saini mkataba wa makubaliano, unaozingatia maeneo mawili muhimu elimu ya STEM na ya kidijitali, lakini pia katika maeneo mengine kama vile kubadilishana, uwezo wa utafiti,” alisema Prof Huang.

Alisema ushirikiano huo pia utaboresha matokeo ya elimu na kuwatayarisha wanafunzi kwa siku zijazo. Na kwamba inaonyesha imani yao katika kuleta mabadiliko ya elimu na azimio la kutoa fursa ambazo ni jumuishi, zinazolingana na zinazotazamia mbele.

“Kwa pamoja, tunaanza safari ambayo inaahidi sio tu kuimarisha maisha ya wanafunzi wetu lakini pia kuchangia ipasavyo katika nyanja pana ya elimu katika nchi zetu zote mbili.

“Kwa utekelezwaji wa mtaala mpya, nina imani kuwa juhudi zetu za pamoja zitaleta matokeo ya ajabu, na kutengeneza njia kwa mustakabali mzuri na wa ubunifu zaidi,” alisema Prof. Huang.

Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt. Aneth Komba akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo cha ZJNU, Prof. Huang Xiao wakisaini makubaliano katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt. Aneth Komba akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo cha ZJNU, Prof. Huang Xiao wakibadilishana mikataba mara baada ya kusaini makubaliano katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt. Aneth Komba akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo cha ZJNU, Prof. Huang Xiao wakionesha mikataba mara baada ya kusaini makubaliano katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt. Aneth Komba akimkabidhi zawadi  ya kinyago cha kimasai Mkuu wa Chuo cha ZJNU, Prof. Huang Xiao kwenye hafla ya kusaini makubaliano katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt. Aneth Komba akipokea zawadi  kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha ZJNU, Prof. Huang Xiao kwenye hafla ya kusaini makubaliano katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University (ZJNU) cha nchini China kwa lengo la kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University (ZJNU) , Prof. Huang Xiao akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa lengo la kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt. Aneth Komba akiwa na Mkuu wa Chuo cha ZJNU, Prof. Huang Xiao wakiapata picha ya pamoja na watumishi wa TET na wawakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University (ZJNU) wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya TET na ZJNU katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya Sayansi. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 10, 2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Previous Post Next Post