TIMU YA ARGENTINA YATWAA UBINGWA WA COPA AMERICA 2024


Timu ya Argentina Yatwaa Ubingwa wa COPA America 2024

Nahodha wa Argentina, #LionelMessi ameiongoza Timu yake ya Taifa kutwaa Ubingwa wa #CopaAmerica2024 kwa kuifunga #Colombia goli 1-0 katika Mchezo wa Fainali


Hadi dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa 0-0, zilipoongezwa dakika 30 ndipo #LautaroMartinez akapatia #Argentina goli dakika ya 112


Argentina ambayo imetwaa Ubingwa huo mara 16 ikiwa ndio timu ililichukua mara nyingi zaidi, imefanikiwa kutetea Ubingwa huo ilioubeba Mwaka 2021 kwa kuifunga #Brazil goli 1-0


Timu zinazofuatia kwa kutwaa Copa America mara nyingi ni Uruguay (15), Brazil (9), Paraguay (2), Chile (2) na Peru (2)

Previous Post Next Post