WALIMU WATATU, MWANAFUNZI NA MUUGUZI KIZIMBANI KWA KUIBA MITIHANI

 MWANDISHI WETU, KAHAMA


Walimu watatu na mwanafunzi mmoja wa shule ya Sekondari Lunguya iliyopo Halamshauri ya Msalala mkoani Shinyanga, Pamoja na Muunguzi mmoja wamepandishwa kizimbati katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama kwa kuhusika na wizi wa mitihani ya kitato cha nne iliyofanyika Novemba 2023.

Washtakiwa hao ni pamoja na Muuguzi Lucy Maganda(39) aliyekuwa akirudia mitihani, Ovan Katunzi(54) mwalimu, Jacob Daniel(36) Mwalimu, Ramson Kanyenyemo(35) Mwalimu pamoja na Paschal Buchanagandi(21) mwanafunzi aliyekuwa akirudia mitihani shule ya sekondari Lunguya.

Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu mkazi wa Wilaya ya Kahama Christina Chovenye,Mwendesha mashitaka wa serikali Jukael Jairo amedai kwamba washtakiwa hao walitenda kola la jina namba 20975/2024 kinyume cha sheria ya baraza la mitihani sura namba 107 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019 kwa kuvujisha mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba mwaka jana.

Jairo amesema kosa la kwanza linawahusu wanafunzi wawili waliokuwa wakirudia mitihani ya kidato cha nne kwa kukutwa na nyaraka zisizohitajika katila chumba cha mitihani kinyume cha kifungu cha sheria namba 20(2) na kifungu cha 24(1)(2) cha sheria ya baraza la mitihani sura namba 107 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Kosa la pili linawahusu walimu watatu wa sekondari ya Lungu iliyopo Halmashauri ya Msalala kwa kuvujisha mitihani wa somo la Jogorafia kwa wanafunzi wakati mitihani ikiendelea kinyume na sheria ya baraza la mitihani sura namba 107 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Jairo amesema kosa la tatu linamhusu mshtakiwa namba mbili Ovan Katunzi ambaye ni mwalimu kushindwa kulinda karatasi za majibu ya mtihani wa Jografia na upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa.

Washtakiwa wote watano wamekana mashtaka yao na kurejeshwa rumande hadi agosti saba shauri hilo litakaposikilizwa tena baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja akiwa ni mtumishi wa umma,Wakiwa na bondi ya thamani ya shilingi milioni tano Pamoja na kitambulisho cha Taifa (NIDA).


Previous Post Next Post