WANAFUNZI 290 WAHITIMU MAFUNZO MBALIMBALI CHUO CHA HILL FOREST SHINYANGA, NAIBU WAZIRI KATAMBI, MEYA MASUMBUKO WAHIMIZA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Jumla ya Wanafunzi 290 wamehitimu kozi mbalimbali wakiwemo  watalamu wa ofisi za mapokezi (front office operation), Waalimu wa kufundisha shule ya Nassary  pamoja na Wasaidizi wa Maabara katika chuo cha Hill Forest Shinyanga kilichopo kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Mahafali ya kumi (10) katika chuo hicho cha Hill Forest Shinyanga yamefanyika  Jumamosi Julai 27,2024 ambapo mgeni rasmi ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akimwakilisha mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi.

Wanafunzi 290  baadhi yao hawakuwa na uwezo na wengine ambao walikosa nafasi ya kuendelea na masamo kutokana na sababu mbali mbali, wamesoma na kuhitimu katika chuo hicho cha Hill Forest kupitia ufadhili wa serikali  na kwamba serikali imetoa ada kwa asilimia mia moja.

 Akizungumza katika mahafali hayo, kwa njia ya simu Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga Mhe. Paschal Patrobas Katambi amesema serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kuhakikisha vijana wote wanaopata mafunzo kwenye vyuo wanapata vifaa ama mikopo ili kuendeleza ujuzi wao huku akiwasisitiza kutokukata tamaa.

“Mimi ahadi yangu kwenu moja ni kuwapenda sana lakini pili ni kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kila mmoja wetu ananufaika na Shinyanga yetu katika uwekezaji na kuleta maendeleo kwenye sekta zote za elimu, miundombinu, sekta ya Afya, sekta ya Kilimo na sekta zingine zote zinazosababisha kuweza kuleta mzunguko wa fedha katika Manispaa yetu ya Shinyanga”.

“Rai yangu kwa wazazi waendelee kutupa ushirikiano na rai yangu kwa wanafunzi wahitimu tuendelee kupambana tuhakikishe kwamba elimu hiyo tuliyoipata itusaidie zaidi katika kuweza kuinua uchumi wetu binafsi lakini pia wa familia zetu na kushiriki katika ujenzi wa taifa”.amesema Mhe. Katambi

“Kuna mifumo ya mikopo ipo tutaendelea kuhakikisha kwamba wale wahitimu basi tunawawezesha kama siyo mikopo basi vifaa ili waweze kufanya kazi na kuitumia elimu hiyo kwa ajili ya ujenzi wa taifa kikutwa msikate tama, tufanye kazi, tupambane usiku na mchana kikutwa tu usihame kwenye malengo yako achana na wale wanaokusema vibaya kukukatisha tamaa wewe angalia mbele hakika utafanikiwa na sisi tunawaahidi kuwatengenezea mazingira wezeshi”.amesema Mhe. Katambi

Mgeni rasmi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewataka wakazi wa Manispaa hiyo kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali zikiwemo fursa katika sekta ya elimu ili kupata elimu na ujunzi ambao utasaidia kujikwamua kiuchumi.

“Serikali imeweka utaratibu wa fursa mbalimbali ambazo vijana wetu wakiweza kuzitumia wataingia kwenye ajira zao binafsi na wanaweza kurejesha fedha ya serikali lakini pia wao wenyewe watatengeneza ajira kwa watu wengine na ndiyo lengo la serikali, kwahiyo nianze kwa kuwapongeza vinaja ambao mmehitimu mafunzo yenu nina amini mtakwenda kuyasimamia maadili yote mliyopewa hapa shuleni ili kuwa faida kwenu na faida kwa taifa  hasa mdumishe nidhamu na kuyalinda maadili mtambue kuwa hakuna mwajiri ambaye anaweza kukaa na mfanyakazi wake ambaye hafanyikazi kwa juhudi lakini pia niwaombe vijana tuchangamkia fursa hasa za kielimu katika Manispaa yetu ya Shinyanga kuliko kukaa nyumbani na wengine kujihusisha kwenye makundi mabaya kama uvutaji sigara, pombe na wengine kucheza michezo ya kubahatisha”.amesema Meya

Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo cha Hill Forest Shinyanga Mhe. John Siagi amemshukuru mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi kwa ushirikiano na juhudi alizozifanya katika kufanikisha ufadhili huo kwa wanafunzi 290.

Siagi ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi ambao wanaishi na watoto nyumbani kuhakikisha wanachangamkia fursa hizo zinazotolewa na serikali

“Niwaalikeni wazazi wenzagu kama tuna watoto wako nyumbani tutumie fursa hizo na ukweli sisi Shinyanga bado tumelala tuamke, watoto tusiwaache wakazagaa tunafursa hizo na kwa bahati nzuri hujachelewa bado wapo wanafunzi watakao ingia hapa intek nyingine ambayo tunaanza kupokea wanafunzi mwezi wa tisa kwahiyo tunawakaribisha Mwezi wa tisa si mbali sana kwahiyo ni kipindi kizuri pia kwanza kufanya maadalizi fomu zipo na kwa bahati nzuri hizi fani tulizonazo hapa tumejipambania sana kwenye soko la ajira kwanza ni fani zenye masoko makubwa sana kwenye ajira”amesema Siagi

Wakizungumza baadhi ya wanafunzi ambao wamehitimu masomo yao wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ufadhili huo huku wakiahidi kutumia ujuzi huo kwenda kuleta mabadiliko chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.

Aidha katika taarifa yake mkuu wa chuo cha Hill Forest Shinyanga, Fortunata Paschal Shine ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio ya chuo hicho huku akiishukuru na kuipongeza serikali kwa kuendelea kutoa fursa kwa vijana.

Chuo chetu cha hill forest kilianzishwa mwaka 2012 enzi hizo kikiwa na kozi mbili ambazo ni wasaidizi wa maabara na watalamu wa ofisi za mapokezi yaani "front office operation, kutokana na uzoefu tulioendelea kuupata toka chuo kimeanzishwa tumeweza pia kuongeza kozi fupi na ndefu ikiwa pamoja na Ualimu wa watoto wadogo, Habari na mawasiliano pamoja na mapishi, chuo chetu hapo awali kilikuwa na vyumba viwili vya madarasa na watumishi wasiopungua wane”.

“Toka kianzishwe,chuo chetu kimesajiliwa na kitamburika na serikali kikiwa chini ya NACTIVET, napenda kutoa shukrani kwa niaba ya uongozi mzima wa chuo chetu, shukran ziende kwa serikali ya jamhuri ya muongano ya Taznzania china ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wasidizi wake wote kwa kutupa kipaumbele na kuamini juu ya fursa hii adimu sana ya mpango wa maendeleo na kukuza ujuzi kwa vijana wa kitanzania, hakika tumeiona ni njema ya serikili yetu ya kuwajengea uwezo vijana wetu wa kuajiliwa na kujiali pia”.

“Lakini nitakuwa mchoyo wa fadhira nisipo kushukuru mbunge wa jimbo la Shinyanga, naibu Waziri wa kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu kwa jitihada kubwa unazo endelea kizifanya za kuwatetea,kuwapambania na kuwawezesha vijana wengi ndani ya jimbo  la Shinyanga mjini na maeneo jirani, napenda kuwajulisha vijana wetu wanao hitimu leo pamoja na wazazi waliopo ya kwamba,bila katambi fursa hii huenda tungeikosa,tunakushukuru sana”.

“Mafanikio  tulio yapata hadi sasa hasa baada ya kupata fursa ya mpango huu wa ukuzaji wa ujuzi ambao umefadhiliwa na serikali kwa asilimia mia moja ya ada ya mafunzo, tumeongeza vyumba vya madarasa hadi kufikia vinane, Tumeongeza walimu hadi kufikia 11 pamoja na watumishi wasio kuwa waalimu 9,aidha tumeongeza ofisi hadi kufikia 14, tumefanikiwa kuwa na mradi wa maji ya kisima na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji kwa matumizi ya wana chuo na kilimo cha mboga na matunda. amesema Fortunata

Tumeongeza udahili kutoka 60 mwaka 2023 hadi 300 mwaka huu 2024, Tumeboresha hali na masilahi ya watumishi wetu; matarajio ya chuo chetu ni makubwa sana kifupi tunataraji kuwa kituo bora cha mwanzo wa maarifa na ujuzi kwa kusudio la kudahili hadi kufikia wanachuo kwa maelfu,kukuza kipato na kuongenza huduma kwa jamii na kushiriki kikamatifu katika harakati za kuipunguzia mzigo serikali juu ya fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania.

Tunaomba serikali iendelee na moyo huu wa dhati wa kuwafadhiri watoto wetu hasa ambao hawana uwezo na wale ambao wamekosa nafasi ya kuendelea na masamo kutokana na sababu mbali mbali ili kuwasaidia wazazi na vijana wenyewe, Lakini pia nakuomba Mhe. Mbuge na naibu waziri utupatie tena fursa hii mradi unao fuata na kama utapendenzwa utuongezee idadi ya wana chuo kwani tunao uwezo wa kudahiri zaidi ya wanachuo 600 kwa mwaka, Vile vile tuwaombe wazazi waendelee kukiamini na kushiriki kukijenga chuo chetu kwa kutuletea vijana ili nia yetu njema tunayo ionyesha kwa utekelezaji iweze kuzaa matunda tunayo yatamani.”amesema Fortunata

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwenye mahafali ya kumi (10) katika chuo cha Hill Forest Shinyanga ambapo jumla ya wanafunzi 290 wamehitimu mafunzo yao.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza kwa njia ya simu na mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi kwenye mahafali ya kumi (10) katika chuo cha Hill Forest Shinyanga.

Mkurugenzi wa chuo cha Hill Forest Shinyanga Mhe. John Siagi akizungumza kwenye mahafali ya kumi (10) Julai 27,2024.

Mkuu wa chuo cha Hill Forest Shinyanga, Fortunata Paschal Shine akisoma taarifa fupi ya chuo cha Hill Forest Shinyanga.

Awali wahitimu katika chuo cha Hill Forest Shinyanga wakiingia ukumbini.

Mkuu wa chuo cha Hill Forest Shinyanga, Fortunata Paschal Shine akikabidhi taarifa fupi ya chuo kwa mgeni rasmi.

Mwenyekiti wa bodi ya chuo, Daniel Emmanuel Manga akizungumza kwenye mahafali ya kumi ya chuo cha Hill Forest Shinyanga.

Mratibu wa mafunzo ambaye pia ni mwalimu wa taaluma katika chuo cha Hill Forest, John Mtaka akiwa katika zoezi la kutoa vyeti vya pongezi kwa wanafunzi ambao wamefanya vizuri.


 

Previous Post Next Post