Dada wa kazi aliyejulikana kwa jina la Clemensia Cosmas (19) mkazi mwenyeji wa Kasulu, Mkoani Kigoma, anadaiwa kumchinja shingoni na kumkata komoreo mtoto wa mwajiri wake Maliki Hashimu(6) maeneo ya Goba kwa Wakutili kisha kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza ,Baba mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa haamini alichokiona kwa mtoto wake kwani amechinjwa vibaya sana, shingo mpaka koromeo limekatwa mara mbili, muda mfupi baada ya kutoka shule, kwani dada huyo alikuwa akitumia nguvu kubwa mtoto alijitahidi kutoka akiwa anamwagika damu nyingi aombe msaada ndio alipodondoka na majirani kumuona.
“Mama yake alipopigiwa simu na majirani alimkuta mtoto kwenye hali mbaya sana na alipomuuliza alimjibu kwa shida dada kanichinja kisha hakuweza kuongea tena” alisema baba huyo.