WATU SABA WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA SHILINGI MILIONI 305 KAHAMA


NA NEEMA NKUMBI -KAHAMA

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu saba, akiwemo meneja huduma kwa wateja na watumishi wengine wawili wa Benki ya CRDB tawi la Kahama, kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha shilingi milioni 305.


Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Kened Mgani amesema kuwa tukio hilo limetokea  Julai 04, ambapo watu wanne wakazi wa Dar es Salaam walifika katika benki hiyo wakiwa na gari dogo aina ya IST na mwanamke mmoja  alishuka na kuelekea kwa meneja huduma kwa wateja ambapo meneja huyo alimkabidhi  kwa muhudumu wa benki ili aweze kuhudumiwa kama wateja wengine.

Kamanda Mgani amesema mwanamke huyo alimhudumiwa kwa  kupewa fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 30 kwa kutumia kadi bandia pia alitaka   kiasi cha shilingi milioni 275 kuwekwa katika akaunti zingine mbili toafuti katika benki hiyo.

Amesema jeshi hilo lilipata taarifa za siri kuhusiana na wizi huo na kuweka mtego wa haraka na kufanikiwa kuwakamata watu hao wakiwa na fedha taslimu milioni 30 huku fedha zingine zikifungiwa zisiende katika akaunti hizo wakati wenzake wakimsubiri nje kwenye gari lao.

Kamanda Mgani amesema uchunguzi  unaeendela ili kubaini mtandao mzima jinsi gani walijipanga mpaka kutaka kuchukua fedha kupitia akaunti ya mtu bila ridhaa ya mtu kwa kutumia nyaraka  na vitambulisho vya kugushi sambamba na sahihi. 
Previous Post Next Post