Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassimu Majaliwa amezihimiza Taasisi za Kidini nchini kuendelea kuimarisha Umoja na Ushirikano na Serikali kama vitabu vitakatifu vya dini vinavyotaka.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jijini Dodoma July 19,2024 wakati akifunga Baraza la Maaskofu wa umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT)liliofanyika kwa siku tatu na kuongozwa na salamu inayosema "Palipo na Umoja,Bwana huanuru Baraka".
Na kuongeza kuwa Serikali inathamini uwepo na mchango wa Taasisi za Kidini kwani Serikali pekee isingeweza kuhubiri Upendo,Amani na Utulivu kwa wananchi wote kwa wakati mmoja lakini kwa viongozi Wadini imekuwa rahisi kwani wanakutana kuanzia Ijumaa,Al Alhamisi na Jumapili.
"Hivyo niwatake Taasisi zote za Kidini kuendelea kuimarisha umoja na Ushirikiano na Serikali pia muendelee kuishi kwa vitendo kwani hata Vitabu vitakatifu vinasisitiza kuishi kwa umoja na kama ilivyo kaulimbiu yenu inayosema "Palipo na Umoja,Bwana huamuru Baraka".
Wakati akitoa salamu za CPCT Mwenyekiti wa CPCT Taifa Askofu Dkt Barbanas Mtokambali ametumia nafasi hii kutoa Rai kwa Serikali kuandaa mazingira rafikikkwa uchaguzi kuwa huru,wazi na haki kwa uchunguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2025.
"Mwaka huu 2024 ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwaka ujao 2025 ni wa uchaguzi wa Raisi,Wabunge na Madiwani. Ni ombi na rai ya CPCT kwamba Serikali iandae mazingira rafiki kwa uchaguzi sio tu huru na haki bali pia unaonekana kweli kuwa ndivyo ulivyo ili wapiga kura wawe na imani na matokeo,na pia waweze kushiriki zoezi hilo muhimu bila hofu wala uwepo wa vitisho au matumizi makubwa vya vyimbo vya Dola".
Na kuongeza kuwa Baraza hili linakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na Ofisi za makao makuu yake ambapo kwasasa wanatumia Ofisi za muda ambazo hazitoshelezi mahitaji ya Baraza hilo.
Awali akisoma taarifa ya Msimamo wa CPCT kuhusu Matumizi ya Visaidizi vya Imani Mchungaji Dkt Baraka Kihoza Katibu Mkuu CPCT amesema kuwa CPCT inatoa Wito kwa Makanisa wanachama na makundi mengine yenye mlengo wa kipentekoste kusimamia mafundisho sahihi ua Upentekoste yasiyochanganya na Visaidizi vya Imani kwani kwa kufanya hivyo hakumpi Mungu Utukufu bali kunaibua sintofahamu katika jamii na hivyo wajikite katika kutoa elimu ya tafsiri sahihi ya Nenobla Mungu kwa njia mbalimbali ikiwemo makongamano.
"CPCT inatoa Wito kwa Makanisa wanachama na makundi mengine yenye mlengo wa Kipentekoste kusimamia mafundisho sahihi ya Upentekoste yasiyochanganya na Visaidizi kwani kwa kutofanya hivyo hakumpi Mungu utukufu bali kunaibua sintofahamu katima jamii. Hivyo Makanisa wanachama wa CPCT kwa kushirikiana na idara za CPCT za Teolojia na Elimu na mafunzo wajikite katika kutoa elimu ya tafsiri sahihi ya neno la Mungu kwa njia ya makongamano kwa walimu wa neno la Mungu na viongozi wanaohudumu Makanisa".
Baraza hili la umoja wa Makanisa ya Kipentekoste lilianzishwa rasmi mwaka 1993,na lilikuwa wanachana 130 lakini hadi wamefikia wanachama 170 na kulikuwa na waumini milioni 1.5 ambapo kwasasa lina waumini zaidi ya milioni 12.