Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Diwani wa kata ya Ndala Mhe, Zamda Shabani ameshinda
uchaguzi wa naibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga uliofanyika katika
ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa
ya Shinyanga ikiwa ni awamu ya pili mfululizo (2023/2024-2024-2025.) .
Awali akitoa ufafanuzi juu ya Mgombea nafasi ya
Naibu Meya Mkuu wa Division ya Utawala na Usimamizi Rasilimali watu manispaa ya Shinyanga Ndg, Pius Sayayi amesema Halmashauri ya manispaa
ya Shinyanga. Mhe Pius Sayayi. Amesema Halmashauri ilipokea jina moja tu la
Mgombea ngazi ya Naibu Meya wa Manispaa, hivyo kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi
jina hilo litapigiwa kura za "Ndiyo" na "Hapana".
Kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi endapo mgombea nafasi husika atakuwa mmoja tu
wajumbe watapiga kura za NDIYO au HAPANA
ambapo mgombea huyo akifikia asiliimia hamsini 50% atakuwa ameshinda
Uchaguzi huo. Amesema Ndu Sayayi Mkuu wa Division ya Utawala na Usimamizi
Rasilimali watu manispaa ya Shinyanga
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo Mwenyekiti wa
Uchaguzi ambaye pia ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Ndg. Amesema Ndugu
Zamda shabani ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia zote.
"Jumla
ya wapigakura ni 19, kura zilizopigwa ni 19, kura za ndio ni (0) kuta zilizo
haribika ni (0) kura za ndio ni (19), hivyo kwa mamlaka niliyopewa Ndugu Zamda
Shabani namtangaza kuwa ndiye Mshindi wa ngazi ya Naibu Meya manispaa ya
Shinyangac". Amesema Ndg Said Kitinga Katibu tawala
wilaya ya Shinyanga.
Sambamba na hayo Umefanyika uchaguzi wa kamati za
kudumu kwa mwaka 2024/2025 ambapo Mhe, Ezekiel Sabo kashinda ngazi ya
Mwenyekiti wa kamati ya Afya, Elimu na uchumi Mhe, Hassan Mwendapole ameshinda
kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Madili Mhe, Elias Andrea kashinga kuwa Mwenyekiti
kamati ya Mipangomiji na Mazingira.
Baada ya Uchaguzi huo Naibu Meya Manispaa ya
Shinyana Zamda Shabani amewapongeza wajumbe kwa kumuamini tena kumchagua nafasi
hiyo kwa mwaka wa pili Mfurulizo.
"Niwashukuru
sana waheshimiwa madiwani kwa kuniamini kunichagua tena ili kuendelea kudumu
katika nafasi hii ilikuwa si rahisi kwa sababu wote tunaweza lakini mimi ndiye
mmeniamini zaidi, ninachomba kwenu ni ushirikiano. Nitaendelea kukusaidia
Msitahiki Meya wakati wowote utakapo nihitaji kukusaidia lakini pia nitatoa
ushirikiano kwa watu wote ili tuweze kuijenga manispaa yetu". Amesema
Mhe. Zamda Naibu Meya.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya
Shinyanga Ndg. Anord Makombe amewataka
viongozi wote waliochaguliwa na waheshimiwa Madiwani kutimiza majukumu yao.