Katibu wa Itikadi,Uenzi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Taifa CPA Amos Makalla, Mchungaji Peter Msigwa,wamefanya harambee ya millioni 5,kwa ajili Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara ,Tundu Lisu kununua gari kwa ajili ya kutembea wakati wa ziara zake za kichama.
Zoezi la harambee hiyo ya limefanyika uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Agosti 15,2024 wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi
CPA.Makala ameona kuna umuhimu wa kumchangia Lisu maana gari analotembelea siyo hadhi ya gari ya Mwanasiasa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,amesema siasa siyo vita.
"Hatupaswi kubaguana kwa dini,kabila sisi sote ni Watanzania tupendane,ndio maana tumeamua kushirikiana wanachama wote kumchangia Tundu Lisu ili aweze kupata gari Chama chetu kina upendo na watu wote
Akizungumza mmoja wa aliyewahi kuwa mwanachama na Mbunge wa CHADEMA amewataka wananchi kutopotoshwa na Siasa za Tundu Lisu na viongozi wengine wa chama hicho, kikubwa waendelee kuiamini CCM ndio ilioshika dola.