Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho Jumamosi tarehe 10.08.2024, ataongoza Misa takatifu ambayo itawashirikisha Wanawake wakatoliki Tanzania WAWATA Jimbo la Shinyanga, yenye lengo la kulitegemeza Shirika la Kitawa la kijimbo la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma.
Bi.Magreth amewaomba WAWATA wote pamoja na waamini kujitokeza kwa wingi katika Misa hiyo, ambayo imelenga kulistawisha na kuliendeleza shirika hilo la Jimbo, lililoanzishwa na Askofu Sangu.