Na Elisha Petro
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto ya
Mwaka 2024, hatua inayolenga kukabiliana na vitendo vya ukatili vinavyoendelea
nchini na kuimarisha ulinzi na maslahi bora ya mtoto.
Marekebisho hayo yamegusa sheria tatu
kuu, ambazo ni Sheria ya Makosa ya Kimtandao (Sura ya 443), Sheria ya Mtoto
(Sura ya 13), na Sheria ya Msaada wa Kisheria (Sura ya 21).
Akitoa maelezo kuhusu Muswada huo leo
tarehe 30 Agosti 2024, Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Maendeleo, Jinsia,
Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum, Mhe. Dorothy Gwajima, amesema marekebisho
hayo yamelenga kuondoa mapungufu yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wa baadhi
ya masharti ya sheria hizo ili kumlinda mtoto dhidi ya vitendo mbalimbali vya
ukatili.
"Mheshimiwa
Spika, Muswada huu wa Sheria unaohusu ulinzi wa mtoto unalenga kufanya
maboresho katika sheria tatu: Sheria ya Makosa ya Kimtandao (Sura ya 443),
Sheria ya Mtoto (Sura ya 13), na Sheria ya Msaada wa Kisheria (Sura ya 21) lengo
kuu ni kuondoa mapungufu na kuimarisha ulinzi na maslahi bora ya mtoto,"
amesema Mhe. Gwajima.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa
Mashirika yanayotekeleza miradi ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Mkoa wa Shinyanga (SHY EVAWC), Jonathan Manyama Kifunda, amepongeza juhudi hizo
na kuomba serikali iendelee kuweka mazingira rafiki kwa taasisi
zinazoshughulikia masuala ya ulinzi wa watoto ili kurahisisha utendaji kazi.
"Tumepokea
marekebisho haya kwa furaha kubwa, kwani ni kitu ambacho tulikuwa
tunakitarajia. Uzoefu wetu katika utekelezaji wa miradi ya ulinzi wa watoto
umeonesha changamoto ambazo zimekosa msingi wa kisheria, na hivyo kuja kwa
Muswada huu kutasaidia sana kurahisisha utendaji kazi wetu, wadau mbalimbali,
na hata serikali kwa ujumla," amesema
Kifunda.
Baadhi ya wadau waliofuatilia kikao cha Bunge la 12, Mkutano wa 16, kupitia Televisheni katika ukumbi wa mikutano wa Rafiki SDO Kitangili, wameipongeza serikali kwa kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto, wakisema kuwa maoni yao yamezingatiwa, na hivyo hatua hiyo itasaidia kuimarisha ulinzi wa mtoto katika jamii na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika yanayotekeleza miradi ya kuzua ukatili kwa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga (SHY EVAWC) Jonathan Manyama Kifunda akielezea lengo la kikao hicho.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika yanayotekeleza miradi ya kuzua ukatili kwa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga (SHY EVAWC) Jonathan Manyama Kifunda akielezea lengo la kikao hicho.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika yanayotekeleza miradi ya kuzua ukatili kwa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga (SHY EVAWC) Jonathan Manyama Kifunda akielezea lengo la kikao hicho.
Mratibu wa mfuko wa Ruzuku kwa Wanawake Tanzania Mkoa wa Shinyanga akimkaribisha Mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika yanayotekeleza miradi ya kuzua ukatili kwa wanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga (SHY EVAWC) Jonathan Manyama Kifunda kuelezea lengo la kikao hicho.