Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi ameipongeza Shule za Musabe kwa kuwawezesha wanafunzi kuiwa na ufaulu mzuri wa mitihani yote ya shule za awali,msingi, sekondari pamoja na malezi mazuri kwa watoto.
Akizungumza Jana kaka Mahafari ya 8 ambapo wamehitimu Wanafunzi Jumla 91 Wavulana 53 Wasichana 38 Mkuu huyo wa Wilaya amesema Nyamagana inajivunia uwepo wake maana shule nyingi zimekuwa na malezi mabaya kwa watoto.
Makilagi pia amewataka wazazi kutekeleza majukumu yao ya kulea watoto kimaadili kwani hatua hiyo inawafanya kukua wakiwa wema kwenye jamii.
Naye Meneja wa Shule ya Msingi Musabe amesema Shule ya Musabe Inapokea watu wote bila kujali kipato chao cha maisha.
Zela Ezekiel Nyandu Ambae Mtoto wake amehitimu Darasa la Saba ameipongeza Shule ya Musabe kwa Ufundishaji Mzuri kwa watoto ambapo alimleta mwanaye Anod akiwa hajui kusoma na kuandika lakini kwa sasa amekuwa akifanya vizuri.