Na Lucas Raphael,Tabora
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nisahati na maji (EWURA) yalengeza masharti ya uanzishwaji wa Vituo vya mafuta Vijijini ili kusogeze huduma Kwa watumiaji wa Nishati hiyo na kupunguza hatari Kwa wale wanaonunua mafuta ya vibaba au madumu.
Kauli hiyo ilitolewa na meneja wa EWURA kanda ya Magharibi Walter Christopha katika Viwanja vya maoneho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja wa Ipuli mkoani tabora.
Alisema kwamba kulengeza masharti hayo lengo ni kuwavutia wawekezaji wenye uwezo wa kuanzisha biashara ya vituo vya mafutapetroli na dizeli nchini .
Alisema kwamba mahitaji wa mafuta ya Petroli na dizeli katika maeneo ya vijijni yanazidi kuongezeka na ongezeko hilo linatokana na kushamiri kwa shughuli za kiuchumi.
Alisema kwamba wanafanya hivyo ili wananchi wengi wapate huduma ya mafuta ya Taa,Dizeli na Prerol nakuachana na Tabia ya baadhi ya watumiaji wa Nishati hiyo kuweka nishati hiyo kwenye madumu Jambo ambalo ni hatari kwa afya na mazingira .
Aliendelea kusema kuwa kitendo Cha kuhifadhi mafuta ndani yakiwa kwenye madumu ni hatari Kwa usalama wa nyumba ,Mali na binadamu.
Hata hivyo meneja huyo wa kanda aliwataka wawekazaji kujitokeza kwa wingi kw ajili ya kuanzisha vituo hivyo ambavyo mahitaji yake yakekuwa makubwa .
Alisema kwamba hadi sasa katika mkoa wa Tabora kuna vituo maeneo ya vijiji vipo 18 mjini vipo 56 hivyo ni muhimu kwa wanaohitaji kuanzisha vituo hivyo wafikie ofisi za Ewura kanda kwa ajili ya maelezo zaidi .
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nisahati na maji (EWURA)kanda ya magharibi inahudumia mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Katavi na Tabora
Aidha aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwanri aliipongeza wizara ya Nisahati kwa kuanzisha ofisi za Ewura kanda ya Magharibi na kushauri serikali itazame upya juu ya kupunguza gharama za nishati mbadala ili wananchi wengi waweze kutumia nishati safi na salama ya Gesi.
Mwanri aliiomba EWURa kuendelea kutoa elimu kwa ananchi mara kwa mara ili waweze kufahamu majukumu muhimu yanayaotekelezwa na Mamlaka hiyo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia wananchi wengi kuachana na kasi ya ukataji miti na kuamini zaidi matumizi ya nishati safi na salama ya Gesi kwa matumizi mbalimbali.