JACMA MINING AND SERVICE COMPANY LIMITED YAWA MKOMBOZI WA WAENDESHA BAISKELI SHINYANGA

Mmshindi wa kwanza kundi A katika mbio za Baskeli Mkoa wa Shinyanga George Zengo Ndimila, mkazi wa Samuye, ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaodhaminiwa na kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE LTD akikabidhiwa ufunguo wa Pikipiki leo Agosti 8,2024.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE COMPANY LIMITED, yenye makao makuu Jijini Mwanza, leo Agosti 8, 2024, imeshiriki kwenye mashindano ya mbio za Baiskeli Mkoani Shinyanga kama sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, Nanenane, ambayo huadhimishwa kila Mwaka.

Mashindano hayo yamefanyika katika uwanja wa CCM Kambarage, ambapo wachezaji wa mchezo huo wa Baiskeli, wanaodhaminiwa na kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE COMPANY LIMITED, wameshiriki na baadhi yao kupokea zawadi mbalimbali baada ya kuibuka washindi katika makundi yao.

Baadhi ya makundi yaliyoshiriki katika mbio hizo ni pamoja na kundi la wanawake, ambao walikimbia huku wamebeba ndoo za maji kichwani huku Makirikiri Joseph akiibuka mshindi wa kwanza ambaye pia anadhaminiwa na kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE COMPANY LIMITED.

Makundi mengine ni kundi la wazee, pamoja na makundi ya vijana: kundi D, kundi C, kundi B, na kundi A. ambapo Makundi haya yalizunguka umbali mbalimbali, ikiwemo laundi 50, laundi 100, na laundi 150 kwa kundi la mwisho.

Washindi wa makundi yote wamepatiwa zawadi zao, ambapo kwa kundi A, mshindi wa kwanza alikuwa George Zengo Ndimila, mkazi wa Samuye, ambaye amejinyakulia pikipiki mpya aina ya SANLG, George Zengo Ndimila ni mmoja wa wachezaji wanaodhaminiwa na kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE LTD.

Wachezaji wengine wanaodhaminiwa na kampuni hiyo ni pamoja na Amosi Zengo, Kashije Kango, Diclopa Nkango, Sindano Makirikiri, Kianza Makirikiri, Mariamu Mwigulu, pamoja na Toroka Uje Ramani.

Kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE LTD, chini ya Mkurugenzi Jackson Lubasha, inajihusisha na uuzaji wa vipuri vya mashine za kuchimba madini kwenye migodi yote nchini Tanzania. Kwa upande wa jamii, imekuwa ikijihusisha na udhamini na ufadhili wa michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, riadha, na mbio za baiskeli kwa wanawake na wanaume kwa ujumla na kwamba hadi sasa, kampuni imekwisha dhamini na kufadhili mashindano mbalimbali katika mikoa yote ya Tanzania.

Baadhi ya waendesha Baiskeli walioshiriki mashindano hayo leo wamemshukuru kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE LTD kwa udhamini wake, ambao umewasaidia kupata zawadi mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kimaisha.

Mwakilishi wa kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE COMPANY LIMITED kutoka makao makuu Mwanza Bwana William Ngassa amewapongeza washindi hao huku akiwahimiza kuendelea kufanya mazoezi ili kuimarika zaidi na hatimaye waweze kuwa wachezaji wa kimataifa katika michezo hiyo ya mbio za Baskeli.

Mwakilishi wa kampuni ya JACMA MINING AND SERVICE COMPANY LIMITED kutoka makao makuu Mwanza Bwana William Ngassa akizungumza.



Previous Post Next Post