KONGAMANO LA MWENGE WA UHURU KWA VIJANA 2024 LAFANYIKA UWANJA WA SABASABA MANISPAA YA SHINYANGA.

Na Elisha Petro - Misalaba Media

Kongamano la Vijana la Mwenge wa Uhuru 2024 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga limefanyika leo jumapili tarehe 11 Augost 2024 katika uwanja wa Sabasaba uliopo Kambarage Mjini Shinyanga kwa lengo la kujifunza mada mbalimbali ikiwemo uongozi bora.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo Mkurugenzi wa shirika la ukombozi wa kijana na mwanamke Youth and Women Emancipation (YAWE) Mkoa wa Shinyanga ndugu Vicent Raurent amewasisitiza vijana kuiishi kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa kutunza mazingira na kushiriki vyema uchaguzi wa serikali za Mitaa.

‘‘ujio wa Mwenge tutanufaika na mengi lakini mimi kupitia kongamano hili na mada ya Uongozi bora niwaombe mkashiriki vyema kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa aidha kwa kugombea au kupiga kura hizo zote ni haki zako lakini tuhakikishe tunakamilisha taratibu zote za kujisajiri kwenye daftari la mpiga kura jambo jingine tukawe mabalozi wa kutunza mazingira kama kauli mbiu yetu inavyosema kuwa tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa taifa endelevu’’

Kwa upande wake Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (ShyCom) mwalimu Saleh Mrisho Sinzya amesema Mwenge wa Uhuru ulianzishwa ili kuondoa giza kwa kumulika mazuri na mabaya ambayo yanafanywa na baadhi ya watu.

‘‘huu mwenge ulianzishwa ili kuondoa giza na falsafa ya mwenge ulipowashwa tu basi ukaanza kumulika mazuri na mabaya yanayofanywa na baadhi ya watu, yote yakaanza kuonekana mfano wanaopinga maendeleo,washiriki wa rushwa na wale ambao sio wazalendo wanchi yetu yaani wanaochochea vurugu’’

 Afisa mradi ICS ndugu Lucy Maganga amefafanua  umuhimu na uhusiano wa Mwenge wa Uhuru katika maisha ya kila Mtanzania kuwa unaimarisha uzalendo.

‘‘vijana huu mwenge unamaana kubwa sana kwetu kwanza unahusiana na uhalisia wa maisha yetu kwa sababu unatujenga sisi sote kuwa wazalendo wa kweli kwa nchi yetu tutaepuka rushwa na kutokujihusisha na masuala ya giza’’

Wakati huohuo Mratibu wa Vijana Shinyanga ndugu John Eddy amebainisha kuwa ujio wa Mwenge wa huru utasaidia kubadili mtazamo kwa vijana wengi ambao hawatambui umuhimu wa Mwenge wa Uhuru ikiwemo kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi.

‘‘kongamano hili limewalenga vijana kwa sababu ndiyo nguvu kazi ya taifa halafu kuna baaadhi yao hawatambui umuhimu wa mwenge kwa mfano tulienda eneo moja hivi mmoja kati yao alipata maswali mengi sana kuhusu umuhimu wa Mwenge kwenye maisha yake bahati nzuri tulimpa Elimu akatambua. Sasa ujio wa mwenge utasaidia kufungua fahamu za vijana ili watambue uhusiano uliopo kati ya Mwenge na maendeleo yetu, unajua kunafursa nyingi sana zinazofichuliwa na Mwenge ikiwemo haki yako ya kupiga kura na kugombea wakati wa uchaguzi wa serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu’’

Baadhi ya vijana waliohudhulia kongamano hilo wameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuandaa kongamano hilo na kuahidi kutumia fursa ya ujio wa Mwenge wa Uhuru 2024 kujifunza namna ya kutumia fursa za kiuchumi,kutunza mazingira na kushiriki vyema uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mkurugenzi wa shirika la ukombozi wa kijana na mwanamke Youth and Women Emancipation (YAWE) Mkoa wa Shinyanga Vicent Raurent akizungumza wakati wa kongamanoMkurugenzi wa shirika la ukombozi wa kijana na mwanamke Youth and Women Emancipation (YAWE) Mkoa wa Shinyanga Vicent Raurent akizungumza wakati wa kongamanoMkufuzi wa chuo cha Ualimu Shinyanga (ShyCom) ambaye pia ni mlezi wa vijana mwalimu Saleh Mrisho Sizya akizungumza na vijana wakati wa uchangiaji wa mada ya kwanza inayohusu uongozi bora.Mkufuzi wa chuo cha Ualimu Shinyanga (ShyCom) ambaye pia ni mlezi wa vijana mwalimu Saleh Mrisho Sizya akizungumza na vijana wakati wa uchangiaji wa mada ya kwanza inayohusu uongozi bora.Afisa Mradi ICS Lucy Maganga akichangia mjadala wakati wa kongamanoMratibu wa Vijana Shinyanga John Eddy akizunguza wakati wa kichangia mada kwenye kongamanoMkurugenzi Fikra Mpya Bi. Leah Josia akizungumza wakati wa kuchangia mada kwenye kongamano

Baadhi ya washiriki vijana wakiwasilisha mada mbalimbali wakati wa kongamano
Previous Post Next Post