Maafisa waandikishaji wasaidizi wakiapishwa
Maafisa waandikishaji
wasaidizi wa jimbo la Uchaguzi Shinyanga Mjini leo agosti 14,2024 wameapishwa
na hakimu Agness Said Mlimbi kiapo cha kutunza siri Pamoja na kiapo cha kutofungamana na chama
chochote cha siasa
Mafunzo hayo na viapo hivyo vimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa lewis Kalinjuna uliopo halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa maafisa hao wasaidizi waandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura jimbo la Shinyanga Mjini.
Awali akitoa
msisitizo hakimu Mlimbi amewasihi maafisa wasaidizi hao kufanya kazi chini ya
Misingi na utaratibu
“Tume huru ya uchaguzi
Imewaamini kuwa mnaweza tufanye kazi chini ya misingi na taratibu” amesema
Hakimu Mlimbi
Naye Afisa mwandikishaji jimbo la shinyanga Mjini Mwl. Alexius Kagunze amewataka maafisa waandikishaji wasaidizi Pamoja na waendeshaji vifaa vya bayometriki kuwa makini kusikiliza mafunzo hayo.
“zoezi lihi sio
la siasa,mimi kama afisa mwandikishaji sitowavumilia maafisa wasaidizi wavivu
na ambao hawatakwenda na taratibu na kanunu za uchaguzi,zingatieni mafunzo haya,kuweni
makini ili mkatende kazi kama ipasavyo”.Amesema Mwl. Kagunze
Mafunzo haya yataendelea kwa siku mbili kwa lengo la kutoa mafunzo kwa maafisa waandikishaji wasaidizi watakaokwenda kusimamia daftari uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo kwa jimbi la shinyanga Mjini zoezi hilo litaanza agoasti 21 hadi 27, 2024.