MBUNGE MASSANJA AMUMIMINIA PONGEZI CHATANDA

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mwanza Mary Massanja ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji mitaji ya Umma amempongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama hicho kutembea eneo hilo.

Pongezi hizo amezitoa jana kufuatia ziara ya Mary Chatanda katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza kutembelea Miradi ya Maendeleo kujionea Utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Amesema hatua ya kiongozi huyo kuchukua jukumu la kutembea Miradi hiyo kujionea shughuli zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ni ya kupongezwa kwani inaongeza ari ya utekelezji wa kazi hizo kwa kiwango cha juu.

"Hii ni hatua ya kupongezwa kwani Chama ni msimamizi wa Serikali iliyopo madarakani hivyo nimefarijika mno kumuona Mwenyekiti kufika kujionea Kwa Macho yake yanayofanywa na Serikali yetu" alisema Massanja.

Massanja alisema Mkoa wa Mwanza Inatekelezwa miradi mikubwa ya kimkakati kwa maendeleo ya taifa ambayo inahitaji kutembelewa na Viongozi wakuu wa Chama kujionea na kushauri Ili iweze kuwa na tija.

Previous Post Next Post