MIRADI 13 YA BILIONI 7.6 YAPATIKANA NA DOSARI, NAIBU WAZIRI KATAMBI AONYA WATUMISHI WA UMMA WALIOHUSIKA, MWENGE WA UHURU WAENDELEA

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza  katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, amesema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbia katika mikoa zaidi ya 22 na kukagua miradi 1,074 yenye thamani ya shilingi trilioni 10.7.

Katika miradi hiyo, miradi 13 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 imekutwa na dosari mbalimbali na kwamba Mwenge wa Uhuru  umepita kwenye Halmashauri 131 na bado unatarajiwa kufika katika Halmashauri 64 kati ya 195 zilizopangwa.

Mhe. Katambi amesema kuwa miradi iliyo na dosari tayari imechukuliwa hatua stahiki na mamlaka husika zimepewa maagizo ya kuirekebisha mara moja.

Miongoni mwa miradi iliyokutwa na dosari ni mradi wa maji katika Manispaa ya Morogoro, pamoja na miradi mingine iliyopo mikoa ya Njombe, Dodoma, Singida, Mara, na Itilima mkoani Simiyu.

"Hadi kufikia leo, tarehe 11 Agosti 2024, Mwenge wa Uhuru tayari umeishakimbizwa katika mikoa 22 kati ya mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo mkoa wetu wa Shinyanga ambao umepokea Mwenge wa Uhuru wilayani Kishapu ukitokea mkoani Simiyu". 

"Katika mikoa hii 22, Mwenge wa Uhuru umefanyia kazi miradi 1,074 yenye thamani ya shilingi 10,676,901,332,349.08 katika halmashauri 131 kati ya 195. Katika miradi hiyo 1,074 iliyofanyiwa kazi, miradi kumi na mitatu (13) imekutwa na dosari na kukataliwa na Mwenge wa Uhuru, ikiwa na thamani ya Tshs. 7,553,085,484.34".

"Miradi hii kumi na mitatu (13) iliyokataliwa ni pamoja na mradi mmoja wa maji katika Manispaa ya Morogoro, miradi miwili (2) Mafia mkoani Pwani, miradi miwili (2) Tandahimba, mradi mmoja Nanyumbu - Mtwara, miradi miwili (2) Tunduru - Ruvuma, mradi mmoja Ludewa mkoani Njombe, mradi mmoja Mpwapwa mkoani Dodoma, mradi mmoja Mkalama mkoani Singida, mradi mmoja katika Halmashauri ya Mji Bunda mkoani Mara, na mradi mmoja Itilima mkoani Simiyu."amesema Katambi

Mhe. Katambi ameongeza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria na kiutawala dhidi ya watumishi wa umma watakaobainika kuhusika na kasoro hizo.

 "Hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria na kiutawala pale ambapo mradi utapata dosari na watumishi wa umma wamehusika," amesema Mhe. Katambi,

Amesisitiza kuwa fedha zilizotolewa na serikali zinapaswa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi bila kuleta hasara yoyote.

Mwenge wa Uhuru unaendelea na kazi zake katika mikoa na Halmashauri zilizobaki, ukilenga kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa inakaguliwa na kuhakikisha inatoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza  katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza  katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Paschal Katambi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini akizungumza  katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa shule ya msingi Ibadakuli leo Jumapili Agosti 11,2024.

TAZAMA HAPA CHINI PICHA ZA LEO KWENYE MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU MANISPAA YA SHINYANGA

Previous Post Next Post