Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey Eliakimu Mnzava, akiipongeza SHUWASA kwa uendelevu mzuri wa mradi wa maji Bugayambelele Manispaa ya Shinyanga.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na hatua
zilizopigwa katika uendelevu wa mradi wa maji safi na salama kwenye kijiji cha
Bugayambelele, Manispaa ya Shinyanga.
Mradi huu, unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), ulizinduliwa mwaka jana kwa lengo la
kuboresha upatikanaji wa maji safi kwa wananchi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey
Eliakimu Mnzava, baada ya kutembelea na kukagua mradi huo ameeleza kuridhishwa
kwake na maendeleo yaliyofikiwa.
Ametumia
nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kulinda miundombinu ya
maji, akibainisha kuwa serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha huduma ya
maji inapatikana kwa wote.
Mnzava ameipongeza SHUWASA kwa uendelevu wa mradi
huo na kuwasihi wananchi kuendelea kulinda miundombinu hiyo.
“Ni muhimu kwa
wananchi kuzingatia jukumu lao la kulinda miundombinu hii ili kuhakikisha
malengo ya serikali yanatimia, na kila mmoja apate maji safi na salama kama
ilivyokusudiwa,” amesisitiza.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Shinyanga,
Angel Mwaipopo, akisoma taarifa ya uendelevu wa mradi huo kwa kiongozi wa
Mwenge, ameeleza kuwa mradi huo unatarajiwa kunufaisha wakazi wapatao 10,165.
“Mradi
huu umesababisha ongezeko la upatikanaji wa maji kwa kaya kutoka asilimia 35
hadi asilimia 60, huku idadi ya kaya zinazopata huduma ya maji ikiongezeka
kutoka 142 hadi 248,” amesema Mwaipopo.
Mradi huu ulisanifiwa na Wakala wa Maji Vijijini
(RUWASA) Shinyanga kwa kuongeza mtandao wa maji kwa kilomita 8.041, ambapo
RUWASA ilijenga kilomita 1.5 na SHUWASA ikajenga kilomita 6.459.
“Mradi huu umewezesha pia ujenzi wa Gati
(Water Kiosk) moja ambalo linahudumia zaidi ya kaya 30 kwa nyakati tofauti,”
Amesema kuwa SHUWASA inapanga kuongeza mtandao wa
majisafi kwa kilomita 2.1 zaidi katika mwaka wa fedha 2024/2025 ili kuwafikia
wakazi wengi zaidi.
Thamani ya mradi huo ni shilingi 279,465,134.40,
ikiwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Wananchi wa Shinyanga wameendelea kuishukuru
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia
Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kutekeleza miradi ya maji ambayo
imepunguza adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendelea katika Manispaa ya Shinyanga, ambapo Mwenge utapita katika miradi kumi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.2, huku ukikimbizwa kwa umbali wa kilomita 74.5.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Shinyanga,
Angel Mwaipopo, akisoma taarifa ya uendelevu wa mradi huo kwa kiongozi wa
Mwenge leo Jumapili Agosti 11,2024.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Shinyanga,
Angel Mwaipopo, akisoma taarifa ya uendelevu wa mradi huo kwa kiongozi wa
Mwenge leo Jumapili Agosti 11,2024.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey
Eliakimu Mnzava, akiipongeza SHUWASA kwa uendelevu mzuri wa mradi wa maji
Bugayambelele Manispaa ya Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey Eliakimu Mnzava, akiipongeza SHUWASA kwa uendelevu mzuri wa mradi wa maji Bugayambelele Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya
Maji safi na usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola
awali akielezea mradi huo unavyowanufaisha wakazi wa kata ya Kizumbi na maeneo
jirani katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya
Maji safi na usafi wa Mazingira Shinyanga SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola
awali akielezea umuhimu wa mradi huo kwa wakazi wa kata ya Kizumbi.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Paschal Katambi akizungumza.