Na Mapuli Kitina Misalaba
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa
darasa la nne shule ya msingi Jitegemee, mkazi wa kijiji cha Maganzo Wilaya ya
Kishapu Mkoani Shinyanga anadaiwa kulawitiwa na kijana mmoja anayekadiliwa kuwa
na umri wa miaka 28.
Akizungumza na Misalaba Media Baba wa mtoto huyo,
Bw. Idd James, ameeleza kwamba mtoto wake ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne
katika Shule ya Msingi Jitegemee, alikuwa akichunga Ng'ombe Jumapili, tarehe 25
Agosti, wakati tukio hilo lilipotokea.
Mtoto huyo alikuwa amekwenda kuchunga kama kawaida,
lakini alipokuwa kwenye majukumu hayo, alikutana na kijana mmoja ambaye alidai
kuwa mtoto huyo Ng'ombe zake zimekula
miti ya nyumbani kwao ambapo mtuhumiwa huyo alimfuata mtoto akamkamata
mkono kisha kumlazimisha kumfuata hadi nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa maelezo ya mzazi pamoja na mtoto
wamesema akiwa nyumbani kwa mtuhumiwa, mtoto alilazimishwa kuvua nguo na hatimaye
alifanyiwa kitendo cha ukatili wa kingono baada ya kutishiwa kwa kisu ambapo baada
ya tukio hilo, mtoto alirudi nyumbani na kumweleza baba yake kilichotokea.
“
Mtoto wangu anasoma darasa la nne shule ya msingi Jitegemee ana umri wa Miaka
11 huwa kuna utaratibu wa kuchunga Ng’ombe siku ambazo siyo za shule Jumamosi na Jumapili sasa siku ya Jumapili
alikuwa anachunga Ngo’ombe badaye kilichotokea katika yale mazingira ambayo
alikuwa anachunga akatokea kijana mmoja kwa kumkadilia anaumri wa Miaka 28 ni
mtu mzima huwa anapiga debe stendi ya mabasi Maganzo akamwambia wewe mbona umelisha miti ya
nyumbani kwetu mtoto wangu akamjibu mbona mimi hata sijafika huko kwenye miti
yenu yule kijana anaishi na baba yake akawa amemshika mkono akampelekea hapo
kwa baba yake ndo akaenda kumwingiza ndani na kumwamlisha avue akiwa amemtolea
kisu kwa vile sasa mtoto ni mdogo akaona
bora asalimishe maisha yake akamsikiliza anavyotaka ndiyo akawa amemlawiti”.amesema
baba wa mtoto Bwana James
Baba huyo alichukua hatua za haraka kumpeleka mtoto
wake kwenye Zahanati ya Maganzo kwa ajili ya vipimo na matibabu ambapo Daktari aliyemhudumia mtoto huyo ni Dkt. Sam
Philip.
Bw. Idd James ameeleza kuwa taarifa za tukio hilo
aliripoti katika kituo cha polisi cha
Maganzo, ambapo polisi walizindua operesheni ya kumsaka mtuhumiwa huyo, ambaye
alikimbia mara baada ya tukio hilo.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bulumbaga, Bw. Nshishi
Jagadi, amesema kuwa amepokea taarifa kuhusu tukio hilo na kutoa wito kwa
wakazi wa kitongoji hicho kushirikiana na polisi katika juhudi za kumkamata
mtuhumiwa.
“Natoa
wito kwa wananchi wangu nawaomba kuanzia mimi ngazi mbalimbali na jamii
tushirikiane na sungusungu kuweza kulinda kitongoji chetu haya matukio ya namna
hii yasijirudie kwa mara ya pili niwaombe wananchi kuwa wanatoa taarifa za
matukioa kama haya ili kuweka kinga kwa watu wahalifu kama hawa wasijirudie
tena”.
"Tunahitaji
kuhakikisha vitendo kama hivi havijirudii tena katika jamii yetu wananchi wote
wanapaswa kushirikiana na vyombo vya usalama ili kudhibiti uhalifu wa aina
hii."amesema Mwenyekiti Jagadi
Mwenyekiti wa Kijiji cha Maganzo, Bw. Charles
Manyenye, ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kuchukua tahadhari zaidi wakati
watoto wanapokwenda kuchunga, na kwamba ni muhimu kwa watoto kutembea kwa
makundi ili kuepuka hatari kama hizi.
“Alinipigia
baba mlezi wa yule mtoto akanieleza taarifa kamili ya tukio hilo kitendo hicho
kwanza kimenikela sana niwaombe tu wazazi kuwa hawa watoto wanapoenda
machungani asiende peke yake wawe wanatembea wawili au watatu kwa sababu
vitendo hivi vinataka kukisili sasa, jamii kwa ujumla wachukue tahadhari kwa
kweli lakini wazazi wawe wanatoa taarifa mapema inapofikia hatua hiyo”.amesema
Bw. Manyenye.
Katibu wa jumuiya ya kupinga ukatili Shujaa wa
Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Wilaya ya Kishapu, Ndg. James
Onyango Meshack, ametembelea familia ya mtoto huyo na kuwahakikishia wazazi
kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.
Pia amewasihi wazazi wa mtoto huyo kuwa karibu na
kijana wao ili kumsaidia kupunguza msongo wa mawazo na athari za tukio hilo.
Misalaba Media imezungumza na baadhi ya wananchi
wakazi wa kijiji cha Maganzo ambao wameliomba hasa jeshi la polisi kufanya
jitihada za kumkamata mtuhumiwa ili hatua za kisheria zichukuliwa.
Katika mwendelezo wa juhudi za kupambana na ukatili
dhidi ya watoto, jamii ya Maganzo imeombwa kutoa ushirikiano na kuhakikisha
kuwa wanatoa taarifa kwa haraka juu ya matukio yanayotishia usalama wa watoto
wao.